Hapa Kazi Tu (HKT) kiwe chama kipya cha kisiasa Tanzania kitakachoenzi falsafa na maono ya Hayati Dkt. Magufuli na kiwe tegemeo la Watanzania

Ni vizuri mmeanzisha chama cha kuigawa CCM. Ndio kifo cha CCM kinaanzia hapo
 
Nini msimamo wa chama chenu tarajiwa HKT kuhusiana na katiba mpya?

Funguka mwanakwetu, wanachama waanzilishi mwaweza anza nao tokea kwenye uzi huu huu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Sisi tunaamini kuwa katiba mpya ni hitaji la watanzania kwa lugha nyingine katiba ni muongo wa nchi unaotakiwa kubadilika kulingana na hitaji la Dunia kwa maana ya kwamba Dunia ya leo sio sawa na Dunia ya enzi za miaka ya 1977 kwa hiyo mambo mengi yamebadilika inabidi pia muongozo wa nchi ubadilike na mabadiliko hayo yaendane na hitaji la kuineemesha Tanzania kwa hiyo sisi tunaunga katiba mpya yenye kuakisi mahitaji halisi ya maisha ya kila siku ya watanzania
 
Mkuu namaanisha Rais hatakiwi kujipendekeza kwa wawekezaji wenye tabia za Carl Peter's, simaanishi Watanzania
Rais kujipendekeza ni nini na rais kuvutia wawekezaji ni nini?

Na unaweza kuwa specific kwa kutaja specific cases na kuacha kujificha nyuma ya generalities?

Na unajuaje unachoita kujipendekeza si kuvutia wawekezaji?

Na mbona hujajibu hoja nyingine?
 

Asante kwa ufafanuzi murua kabisa. Wengi wenye vyama na wasiokuwa na vyama wana mtazamo kama ninyi.

Hii inanirejesha kwenye mada inayojaribu kuangalia kiuhalisia ni wapi tunapopishana kiasi cha kujikuta hatuonani vyema macho kwa macho.

Tulijinasibu kukuomba rasmi kutupa ufafanuzi wako kwenye mambo ya msingi ambayo pia tunadhani huenda labda ni kwa sababu kushindwa kufahamiana vizuri tu:


Ufafanuzi wako ikikupendeza tafadhali.
 
Kwa mfano mkuu utata wa Mradi wa Bagamoyo inabidi pia wewe mwenyewe ujiulize kwa nn CHINA kila akiingia mikataba hii na nchi nyingi huishia kuzinyonyoa chukulia mfano SRI LANKA, ZAMBIA, KENYA zimeelemewa na mzigo wa sera za kiuwekezaji za Mchina huu mradi tungeuweza hata sisi trillion 23 tungeweza kuujenga hata kwa miaka 10 na ukaisha Tuna Bandari kibao ni sawa sawa na ww kuwa na TV ya sebuleni unang'ang"ana kununua TV ya chumbani matokeo yake unaongeza liabilities
 
Hapana mkuu nakuomba sana uelewe kuwa Mzee Magufuli alikuwa muungwana sana ni binadamu aliyekuwa na Mapungufu yake lkn kiukweli Mzee huyu alijitoa kwa ajili ya Tanzania
Tuonyesheni kwanza waliomshambulia lisu azoli watekaji wa mo mwana Zimbabwe nk pia mawazo
 
Hahaha...mtapata taabu sana, yajayo yanafurahisha.
 
Mimi binafsi kama binadamu niliye na ndugu jamaa na marafiki ningependa tuishi kwa upendo kutofautiana kihoja ni jambo la kawaida kwenye maisha na kiukweli siungani na ninalaani matukio ya kuuwawa NA kuteswa watanzania wenzangu enzi za Magufuli hayo yalikuwa mapungufu yake ambayo yawe yalikuwa na baraka zake au hayakuwa na baraka zake yeye kama baba yetu namba moja alistahili kulaumiwa haya yalikuwa mapungufu ya JPM lkn hili haliwezi kufifisha ukweli kwamba Hayati Dkt John Pombe Magufuli baba huyu alikuwa na nia njema na Tanzania kama binadamu tumsameheni kwa makosa yake tuchukue yaliyo mema
 
Mradi wa Bagamoyo hauwezekani kujulikana uzuri wake au ubaya wake mpaka mkataba uwekwe wazi.

Mpaka sasa, kama mradi unaendelea bila kuwekwa wazi, hilo si jambo zuri

Hata hivyo, kuanzisha chama kipya sioni kutasaidia nini na kutabadilisha kipi katika mfumo uliopo.

Mimi nilishaandika umuhimu wa kuweka mikataba wazi tangu mwaka 2011.

Soma hapa.

 
Hapana mkuu nakuomba sana uelewe kuwa Mzee Magufuli alikuwa muungwana sana ni binadamu aliyekuwa na Mapungufu yake lkn kiukweli Mzee huyu alijitoa kwa ajili ya Tanzania

Alikuwa rais muovu na katili. Anzisheni hicho chama uone hata kama mtawezs kuwashinda TLP ya Mrema.
 
Hahaha...mtapata taabu sana, yajayo yanafurahisha.
Hapana hatuwezi kupata taabu tunenee mema kwa manufaa ya nchi yetu ya Tanzania na wewe kama mtanzania mwenzangu nakuomba umsamehe Hayati Dkt Magufuli kwa mapungufu yake kama binadamu tuchukue mema yake yanayoweza kuivusha nchi yetu ya Tanzania hata wewe hapo ndugu yangu haujakamilika hiki chama ni Cha watu wote hakitakuwa na lengo la kumkomoa mtu hiki chama ndicho tegemeo la Watanzania
 
Nitakuwa mwanachama wake.
 
Alikuwa rais muovu na katili. Anzisheni hicho chama uone hata kama mtawezs kuwashinda TLP ya Mrema.
Kaa chini tafakari ndugu yangu utagundua kuwa Dkt Magufuli alikuwa ni binadamu mwenye nia njema na nchi hayo unayoyasema hutokea kila awamu tuunganeni kuenzi falsafa njema za kuikomboa Tanzania kutoka kwenye mikono ya kinyonyaji
 
Sawa kabisa mkuu. Hata mimi nitakuwa mwanachama wako.
Lakini je: -
(1) Una uzalendo na ujasiri wa kweli kutoka moyoni kama alivyokuwa JPM?
(2)Unaumizwa kutoka moyoni unapoona Tanzania inarudi kwa kasi mikononi mwa mafisi?
(3)Upo tayari kujitoa sadaka kwa maneno na matendo kwa kukemea na kulinda rasilimali za Taifa kwa manufaa ya Watanzania kama alivyokuwa JPM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…