Hapa Kazi Tu (HKT) kiwe chama kipya cha kisiasa Tanzania kitakachoenzi falsafa na maono ya Hayati Dkt. Magufuli na kiwe tegemeo la Watanzania

sana kabisa mimi alipokufa Magufuli nilimaliza wiki nzima sitoki nje nilisafiri kwenda chato kumuaaga na kumzika kwa hiyo basi mm maisha yangu yote nitajitolea kutetea mema ya Tanzania kwa kuenzi ndoto falsafa na maono ya JPM
 
Kaa chini tafakari ndugu yangu utagundua kuwa Dkt Magufuli alikuwa ni binadamu mwenye nia njema na nchi hayo unayoyasema hutokea kila awamu tuunganeni kuenzi falsafa njema za kuikomboa Tanzania kutoka kwenye mikono ya kinyonyaji

Nasema hivi, hatujawahi kupata rais muovu wa aina yake, na aliendekeza siasa chafu sana, huku akiua na kuwaacha wakosoaji wake na vilema vya maisha. Usitake hata kutukumbusha ukatili aliyotufanyia yule mtu muovu. Kaunganeni nyie mliofaidika wakati wa ukatili wake.
 
sana kabisa mimi alipokufa Magufuli nilimaliza wiki nzima sitoki nje nilisafiri kwenda chato kumuaaga na kumzika kwa hiyo basi mm maisha yangu yote nitajitolea kutetea mema ya Tanzania kwa kuenzi ndoto falsafa na maono ya JPM
Usingeacha kuumia maana ulikuwa kwenye kundi lake la watu wasiojulikana.
 
Faraja namba moja ni uhuru wetu wa kutoa maoni na mama ameshafanya hivi,labda ninyi mnatafuta faraja ya kuendelea kuwateka watu na kuwasabaya
 
Ukiwa ndani ya CCM hauwezi kuikosoa na kuisahihisha kwa sababu never outshine your master lkn ni rahisi sana kupush ajenda nje ya CCM kuna mwafizikia Newton aliwahi kusema nguvu ya ndani haileti mwelekeo bali ni nguvu ya nje mm nimezaliwa kusimamia ukweli lkn sio kujipendekeza ili nipate madaraka kwangu mm furaha yangu ni kuona matokeo
 
Sawa.

Wewe utafanya kipi tofauti ambacho walio upinzani wameshindwa?

Maana hutakuwa wa kwanza kuanzisha chama tofauti na CCM.
 

Ninakushukuru tena kwa kauli za kitu uzima hizi ulizozitoa:

1. "Magufuli hayo yalikuwa mapungufu yake ambayo yawe yalikuwa na baraka zake au hayakuwa na baraka zake yeye kama baba yetu namba moja alistahili kulaumiwa."

2. "haya yalikuwa mapungufu ya JPM lkn hili haliwezi kufifisha ukweli kwamba Hayati Dkt John Pombe Magufuli baba huyu alikuwa na nia njema na Tanzania."

3. "kama binadamu tumsameheni kwa makosa yake tuchukue yaliyo mema."

Ninakubaliana nawe 100%.

Amini ninakwambia makelele mengine unayoyasikia ni kushindwa kufahamiana tu. Kwa hakika kuanzia leo ninao mtazamo tofauti kabisa kukuhusu wewe na kumhusu hayati Magufuli. Jambo la kheri kabisa, au vipi?

Tukubaliane:

1. Kumsamehe hayati Magufuli.
2. Kuwawajibisha waliomfanya yeye kubeba lawama hizi.
3. Tushirikiane sote kuujenga umoja wetu ikiwamo kudai katiba mpya kwa amani na kwa pamoja

Au unaona je mpaka hapo?
 
Mimi kama Mtanzania nalaani matukio yote yenye nia ovu yaliyofanyika enzi za Magufuli lkn tuchukueni mazuri tuyafanyie kazi HKT Itajitoa kwa wivu mkubwa Sana kutetea Rasilimali za nchi ya Tanzania
Hatutaki tena kurudi utumwani mwashetani hata wewe nakushauli acha kuabudu lishetani *Magufuli ni dude ambalo tutalijutia maisha yetu yote
 
Wewe ni mwanachama wetu mzuri sana wa HKT jiridhishe vizuri kabisa ukiwa umetulia na hoja zako tutaelewana vizuri
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta
Yamekuwa hayo tena!yaani kwa taarifa yako wananchi wengi /wapinzani walikuwa wanaomba jiwe atoke tu, hata kitawale kiumbe chochote tu kile, tutakiunga mkono, ila siyo jiwe, kumbe MUNGU NAYE FUNDI!!Mama hata atawale tu hadi hapo tutakapo pata katiba mpya haina shida kabisa, madamu KINYAMKELA HAKIPO ROHO KWATU!!sasa mama ni upendo tu hata kama hajafanya la maana sana lakini hatufokewi, na tuna amani.
 
Humu watakutukaneni sana, register hiko chama then ingieni field huko muune mitaa itavyowashangaza watu...R.I.P JPM!
ah wapi. kwa kizazi hiki cha wabongo.. kizazi hiki ambacho wakitishiwa na polis kidogo wanarudi ndani?
labda kizazi kingine. ila kama ni kazazi hiki asiweke iman sana kwa watanzania.

kuitoa ccm si cake walk job
 
Ni kweli kwa yeyote aliyekuwa kwenye Taasisi ya Urais enzi za Magufuli na alitenda jinai nadhani mamlaka za dola zikijirisha sheria ichukue mkondo wake lkn si kwa kuwaonea watu, kuhusu katiba mpya hili linatakiwa kuwa mjadala mpana utaoleta majawabu ya kudumu ya Hali za watanzania katika sehemu zao za mashambani, mashuleni, mahospitalini, mimi yeyote anayeinenea mema Tanzania ni rafiki yangu na tutashirikiana naye
 

Asante sana sina zaidi nikuombe tu, tusaidiane kudai katiba mpya tuijenge Tanzania yenye haki, usawa na ustawi kwa manufaa yetu sote, watoto wetu na hata watoto wa watoto wetu.
 
Mbona Zitto aliweza? Mwache ajaribu
 
Nigrastratatract ,

..msimamo wa chama chenu kuhusu tume ya uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa ukoje?

..je, mnadhani tume ya uchaguzi iko sawasawa, au kuna mabadiliko mnadhani yanahitajika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…