KERO Hapa Mbuyuni-Salasala, Dar kuna baa mpya inakera kwa kelele mpaka usiku wa manane

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Mbuyuni-Salasala, Dar es Salaam. Kuna baa mpya imeanzishwa takribani miezi miwili na nusu iliyopita, ikiwa kwenye ghorofa, na imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa maeneo ya jirani.

Muziki unaopigwa kwa sauti kubwa huendelea hadi usiku wa manane, hali inayofanya iwe vigumu kupata usingizi. Nimejaribu kumtafuta Mwenyekiti wa Mtaa kuhusu suala hili, lakini hali imeonekana kuwa mbaya zaidi kana kwamba baada ya kutoa malalamiko, kelele zimeongezeka.

Starehe ya baadhi ya watu imegeuka kuwa kero kwa wakazi wengine.

Baa hiyo inaitwa China Bar, ipo baada ya kuvuka tuta la kwanza kwenye njia ya Salasala inayotokea Bagamoyo Road. Naomba mamlaka husika ichukue hatua kuhakikisha kelele zinadhibitiwa na haki ya wakazi kupata utulivu inalindwa.
 
Pole mkuu, tafuteni no ya RC Chalamila, kama aliweza kuwafungia TIPS Mikocheni, hao ni vifaranga tu,

TIPS ya watoto wa kishua walikuwa wanakula mayi hadi asubuhi, ukipita sasa hivi kimyaaa sana
 
Back
Top Bottom