Hapa ndipo utagombana na unaweza Kuua mafundi wa Kitanzania

Hapa ndipo utagombana na unaweza Kuua mafundi wa Kitanzania

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Huyu ni mtaalam kupiga rangi. Watu kadhaa walinielekeza kwake.gari ambayo inatakiwa kupigwa rangi ni kubwa. Actually ni katika tu kubadilisha rangi iendane na gari nyingine ilizozikuta.

Gari alinambia siku 4 itakuwa tayari.maandilizi n.k.haikuwa na pa kunyooshwa.akanambia atakuja kupigia hapa hapa gari ilipo.

Ameiandaa kwa kutumia vijana wake mara kadhaa. leo ni siku ya 6 ndo kaanza kupiga rangi.tuliandikishana 4 days.akataka nimpe advance. Nlimkatalia sana.maana ni sawa na mtu kutaka fungua duka atuuzie vitu but before sisi wateja tumpe pesa ya kuanzia mtaji.

Wife akatumia busara akasema basi angalau katika tsh 1,800,000. Nimpe hata 800,000. Nikampa 200,000 anunue materials n.k but aongezee za kwake.mimi nlitaka anikabidhi gari nimkabidhi pesa.

Leo siku ya 6 nmerud ameanza kupulizia rangi.kilichonikatisha tamaa ni ktk uchanganyaji wake. Sioni kama anazingatia vipimo vya thinner na kimiminika kingine sikifahamu na rangi yenyewe.anamimina tu kuchanganya anapuliza.

Namuuliza anajuaje ratio yake.anajibu kirahisi."tulia tu boss utaona mwenyewe kitu kinatoka kama ndo kimetoka leo kwa mwingereza"

Nimemwambia aachane na gari yangu aondoke maana naona anafanya masikhara.nlitegemea angekuwa na mchanganyiko unaofuata vipimo.

Lets say.

Rangi Lita moja
Thinner nusu lita
Na xxxxx robo au nusu lita.

Haipo hivyo.anachukua tu anamimina na kule anachukua anamimina anaweka kwenye kopo anapuliza.

WASIWASI WANGU.

inawezekana kusiwe na uwiano sahihi wa rangi au uimara wa rangi sababu mchanganyaji anachanganya kwa macho tu.

Pia alishavunja makubaliano /mkataba.nimemwambia aache gari abebe vyake tuagane kwa amani.hajaamini mpaka nlipoonesha sitanii.

Jambo hili ni tatizo kwa aina nyingi za mafundi tz.hawajali kabisa profession yao.ujanja ujanja tu mwingi wakituibia in kind.binafsi napinga sana jambo hilo.

Natafuta garage nzuri ambayo wanapiga rangi kitaalamu na bei zao ni nzuri standard siyo za kuanza kuimbishana.ila la muhimu wakisema gari uje kuchukue jumatano saa tano nikienda nikalipe nikague gari nichukue.

Hbr za msiba na ugonjwa mimi hazinihusu.
 
Wakati mwingine matatizo tunayaleta sisi mabosi. Kama ulimwamini katika kutafutatafuta yako ya hao mafundi bora wa kupiga rangi ukampata huyo unaona ugumu gani kumpa advance ya 800,000?

Hiyo 200,000 itamsaidia nini ukilinganisha na gharama za aina mbalimbali za rangi za kuchanyanya kupata ratio kamili ya rangi ya gari lako? Kwani yeye huyo jamaa ni kampuni kusema ana mtaji wa kutosha kufanyakazi amalize ndo alipwe?

Wangapi wanazungushwa na kutapeliwa baada ya kumaliza kazi? Wewe ndo umefanya kazi yake iwe ngumu kwa kutompa advance!
 
We jamaa mswahili sana, eti umpe pesa apate mtaji? Daah obvious lazima umpe pesa akanunue material unadhani yeye anamtaji kiasi gani hadi usubiri kazi iishe ndio utoe pesa. Mimi nakushauri achana na mafundi kanunue mwenywe material then piga rangi gari yako itapendeza zaidi.
 
Nadiriki kusema wewe ni mshamba ungemwachia kazi ake afanye amarize akukabiz then ndo utoe dukuduku lako,kwanza huyo kakuvumilia sana sie wengine tungeacha ujadiriane na mkewako Kwanzaa ndipo uje kwa nidham
 
  • Thanks
Reactions: R.K
Ni bora aiseee.... Mimi ufundi wa kiswahili sipendi. Material kanunue kwa pesa yako. Mimi nakupa gari unakamilisha unanikabidhi nakukabidhi pesa.

Nadiriki kusema wewe ni mshamba ungemwachia kazi ake afanye amarize akukabiz then ndo utoe dukuduku lako,kwanza huyo kakuvumilia sana sie wengine tungeacha ujadiriane na mkewako Kwanzaa ndipo uje kwa nidham
 
Zipo na ndo nazitaka hizo. Basi tu nlishawishika nikiambiwa jamaa yupo vizuri. Fundi gani hata usafiri hana?inakatisha tamaa sana.

Ninyi ndiyo mabos longo longo.

Kama uliona hii kazi una ujuzi nayo si ungefanya mwenyewe?

Ni gereji gani unawaachia gari bila kuacha advansi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fundi anatetewa kwa kumchukia mwenye gari.
Fundi ana makosa, alitakiwa aandae badget ya hiyo kazi, kama mtaji hautoshi angemshirikisha mwenye gari kiasi kilicho pungua. Kama mwenye gari akikataa kuongeza hicho kiasi, fundi hatakiwi kuing'ang'ania kazi, tena anamwambia kabisa tajiri "sitaki kuharibu taaluma yangu, tafuta fundi mwingine".
Mafundi wengi wanaendekeza (samahani kwa kauli hii) njaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa utakuwa wa kanda ya ziwa mkuu...sio kwa ujuaji huo mkuu...wakati mwingine jaribu kumuamini mtu akufanyie kazi azingue umzingue.
 
Komeo Lachuma,
Ukitaka vitu systematic vilivyonyooka na vya viwango ni gharama.
Tatizo pia watanzanja wengi wetu tunapenda vya gharama rahisi, halafu bado tunategemea viwango vile vile vya ubora wa juu... Hivi vigu huwa mara nyingi haviendi pamoja (uhusiano wake ni inversely proportional).

Unaweza kukuta hapo hadi mnaafikiana nei uli bargain hatari kabisa, labda alianzia hata 2,800,000. Ukamshusha na kumshusha na kumshusha hadi mkagota kwenye 1.8m.

Kama hukubargain sana hiyo bei, nisamehe mkuu kwa kuja na assumption ambayo si sahihi.
Otherwise, kama unataka viwango tafuta sehwmu standard kweli kweli, na usiogope gharama.
Yote kwa yote,pole sana mkuu kwa usumbufu na kwa kupoteza ur hard earned cash.
Komeo Lachuma
 
andjul,
Jamaa kasema fundi kaomba advance mkuu....si angempa hiyo advance then asikilizie kazi...mambo mengine tunajitakia tu
 
Wengi wanawachukia sana wenye magari. Mimi sipendi kazi za kiswahili.huwa nakataa kutoa advance so fundi aamue kufanya au kutofanya. Ufundi wa ujanja janja sipendi. Nampa kazi fundi na tunapeana mashart.ndo maana huwa hata sipendi ku negotiate ili kila mtu asipate kisingizio.afanye kazi yangu anikabidhi ikiwa tayari nimlipe.

Unaweza niona mkorofi but ni utaratibu tu maana sometime unakuta fundi kaharibu kitu na advance kachukua maumivu mara mbili.

Fundi anatetewa kwa kumchukia mwenye gari.
Fundi ana makosa, alitakiwa aandae badget ya hiyo kazi, kama mtaji hautoshi angemshirikisha mwenye gari kiasi kilicho pungua. Kama mwenye gari akikataa kuongeza hicho kiasi, fundi hatakiwi kuing'ang'ania kazi, tena anamwambia kabisa tajiri "sitaki kuharibu taaluma yangu, tafuta fundi mwingine".
Mafundi wengi wanaendekeza (samahani kwa kauli hii) njaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIKU BARGAIN ILI NISIMPE SABABU YA KUHARIBU KAZI YANGU. NILIMWAMBIA FUNDI SINA MUDA WA KUBARGAIN ANITAJIE BEI YA MWISHO AANZE KAZI.PESA NTAMKABIDHI AKIKABIDHI GARI IKIWA KWA KADRI YA MAELEZO NLIYOMPA TENA KWA KUMWANDIKIA.


Dr. Wansegamila,
 
Nlimwambia fundi
1. Anitajie bei ya mwisho tusipotezeane muda kubargain.

2. Akague gari aniahidi lini atanipa gari ikiwa imekamilika.ataje siku ambayo na excuses zote zitakuwa included. Akanambia siku hizo.alinambia ile gari siku 3. Nikamwambia nampa na nyongeza.

Then nikamwambia pesa yake ntamkabidhi anaponikabidhi gari.

Kesho yake ananambia anataka advance. Ya nini?mbona hajanya kazi advance? Huo ni uhuni. Ujanja ujanja.
 
Back
Top Bottom