Hapa ndipo utagombana na unaweza Kuua mafundi wa Kitanzania

Jamaa anashindwa kutofautisha biashara anadhani ni kila biashara inakopesheka, na kwa ugumu wa mazingira aliyoweka watamchanganyia hata rangi ya nyumba
 
Ni bora ulipe pesa mingi upeleke gari kwa fundi mwenye nidhamu ya kazi na anayejua nini anafanya!

Najaribu ku imagine alivyokuwa anachanganya hizo rangi kama dawa za mitishamba! Ningekuwa mimi ningemtandika na vibao!
 
Komeo Lachuma, kwa nini mlikubaliana apakie rangi nyumbani kwako? Maana kwa uzoefu wangu, rangi ili itoke vizuri lazima ipakwe kwenye a controlled environment. Kusiwe na upepo, jua wala vumbi. Sasa sijui wenda kwako kuna hayo mazingira, ila kwa kawaida bila mazingira hayo niliyotaja hapo juu ni vigumu kutegemea kazi nzuri.
 
Yani Mkuu... binafsi nimekuelewa sana na kwa maelezo yako.... kosa lako ni moja, ukipenda mambo straight kama hivi nenda kwenye maeneo standard.

Hawa mafundi wa mtaani wengi ni magumashi... hata wale wanaojua kazi bado wanafanya kwa uswahili sanaaaa...

kuna mmoja nlimkimbiza baada ya kukuta anachomelea Geti langu bila miwani... akitaka kuchomelea anaangalia pembeni....

nkamuuliza hivyo unaonaje unachofanya? akaniambia "we tulia uone"..., nkamuomba aache kazi muda huo huo maana angeharibu hasingenilipa.. hivyo hasara ingekua kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaona majibu yao? Wanarahisisha sana mambo wakati watu tunatoa pesa.mimi huyu fundi jamaa zangu ndo wamemletea wakimsifia sana.sasa nmeamua kutafuta tu garage inayojielewa.sitaki maneno na mtu.tusije wekana ndani kwa makosa tofauti tofauti.

 
Yaani wewe mwenyewe ungepoteza imani kabisa. Hamna kipimo.anachanganya anavyoona tu inafaa.anachukua rangi anamimina kweye kopo anachukua kimiminika flani kwenye chupa ya maji anamimina akikadiria.then anachukua kingine nacho kwenye chupa ya maji anamimina.anakoroga anaenda kupuliza. No way....hiyo si sawa.


Ni bora ulipe pesa mingi upeleke gari kwa fundi mwenye nidhamu ya kazi na anayejua nini anafanya!

Najaribu ku imagine alivyokuwa anachanganya hizo rangi kama dawa za mitishamba! Ningekuwa mimi ningemtandika na vibao!
 
Mkuu shida ilianzia hapo.nami najua kuna vyumba maalum. Jamaa aliyemleta namheshimu sana alisisitiza gari itatoka kama ndo imetoka UK leo.nilimwambia hbr za unyevu,jua ,mvua pale home maana ni nje.akajibu jamaa anayafahamu yote.yaani mashaka naye yalianza mapema sana....


 
Bwana wee wanakera acha nxio maana tunawapa kazi wachina sometimes..... Kuna fala mmoja nimempa kazi na advance ya material kacbukua lakini kazi haiendi basi tabu tupu... Unamuuliza tabu nini anakodoa mimacho tuu.
 
Mtoa mada una matatizo ya ule uboss wa kisenge. Watu wanaojali standard kama unavyotaka wewe huwezi peleka gari gereji bubu. Eti unamwita Fundi apake rangi nyumbani kwako, harafu unalaumu quality. Gereji bora zipo wachina wenye gereji bora wapo huko temeke wewe unatafuta mafundi wa chini ya mti. Hela huna then unaleta mazarau
Acha ushamba, wenye standard zao wanajua gereji bora sio Kama wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Pole kwa usumbufu uliokumbana nao.
Bongo ukitaka quality utasubiri sana! Asilimia kubwa ya mafundi ni makanjanja, ujanjaujanja mwingi na pia sio waaminifu!!
 
Pole fundi.sasa si ungesema hayo toka mwanzo kwa nini you assured me that you were an expert?

 
ambayo wanapiga rangi kitaalamu na bei zao ni nzuri standard
Tatizo liko hapa,

Kama unataka kupigiwa rangi kitaalamu bei usiiweke kama factor.

Wewe tafuta gereji wanayopiga rangi kitaalamu kwa gharama yoyote ile, utafurahi na roho yako.

Mtu anakuja kupigia rangi nyumbani? Vumbi na contaminants nyingine hazingatii?

Nenda sehemu gari inapigwa rangi kwenye clean room. Nakuambia utafurahi na roho yako na invoice yake pia itakufurahisha
 
[emoji119][emoji119][emoji119]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…