Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Mobutu hana akili,miaka yote hiyo aliyokula. Angestaafu kwa kupenda wala hiki kijiji kisingedhalilika namna hii.
Angestaafu mwenyewe kirahisi afungwe au afilisiwe?

Alijenga maadui wengi wakati alipoingia ikulu na muda wote wa utawala wake.

Watu wa chama cha Patrice Lumumba walikuwa na hasira nae kwa kumuuwa comred wao.
 
Wewe ndugu una chuki mbaya sana.
Huwezi mlinganisha fisadi Mobutu na Magufuli, chuki hiyo inakupeleka pabaya.
 
Mi najiuliza hizi pesa kwanini zisingepelekwa kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza,uwanja wa ndege wa Mwanza hauna hata jengo la Abiria yaaani ni kubanana tu
 
Mobutu pia alikuwa na wapambe wa kumtia moyo lakini alipofukuzwa madarakani wote waliyayuka.
Sisi wengine huwa tunapenda kuwa 'neutral observers' muda mwingi. Nakuomba tu, kwa uzi huu 'specifically', jaribu kulinganisha Gbadolite na Chato ukizingatia 'ACCESSIBILITY', 'POTENTIAL' ya utalii na uchumi kwa ujumla wake, POPULATION ...... etc etc!
 
Ni kuwa hakuna faida za kiuchumi kufanya hivyo.
Wakongo walishindwa kuyataifisha na kuyaendeleza haya makazi ? Nafikiri hata serikali za sasa nazo zina matatizo kichwani. Hiyo ni pesa ya walipa kodi inateketea !
 
Kaa huko na ndoto zako za kupenda kula pesa za wananchi. Na bado... mtaisoma namba hadi mnyooke
Biibiii😂skamoooo
Nakuja na zawadi yakoo nisubiri
1147782
 
Charity begins at home! Uzuri ni kuwa chato ipo Tanzania! Kama malalamiko yanayoelekezwa kwa Mkuu yanalenga kutuaminisha kuwa Chato hapana hadhi katika Tanzania, ama basi yaliyofanywa huko yalipaswa kufanyika kaskazini tu itakuwa ni kumuonea mkuu.
Sawa,Chato ni Tanzania; na Gbadolite ni sehemu ya Zaire (sasa DRC) pia,lakini leo hii pako kama alivyopakusudia Mobutu?

Historia inatabia ya kujirudia.
 
Mobutu Sesseko Kuku ngendu Wazabanga baada ya kuingia madarakani kimabavu akaanza utawala wa kidikteta

Akajenga ikulu/kasri kubwa kijijini kwao Gbadolite ,akajenga uwanja mkubwa wa kutua ndege tena zilikua zile Concord ,uwanja huu alijenga kijijini kwao

Mobutu alipandisha hadhi kijiji cha kwao na kuwa jiji yani jiji la Gbadolite

Mobutu baada ya kufurumushwa madarakani kijiji kimebaki gofu malisho ya mbuzi na ng'ombe

Ikulu imabaki magofu na makazi ya popo

Uwanja wa ndege umebaki kutua ndege john na wengine walio umbwa na Mungu

Mobutu alikula sana hela za Nchi ya Zaire kujitajirisha na kujenga kwao

Leo hii kwao kumebaki magofu

Magufuli soma historia.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gbadolite
IkuluView attachment 1147267View attachment 1147269View attachment 1147270View attachment 1147271View attachment 1147272
[/QUOTE waafrica wakipata uongozi wabinafsi sana wajiangalia wao na matumbo yao na kwao hawajali wengine
 
Sawa,Chato ni Tanzania; na Gbadolite ni sehemu ya Zaire (sasa DRC) pia,lakini leo hii pako kama alivyopakusudia Mobutu?

Historia inatabia ya kujirudia.
Sasa shida ni ya Mobutu ama wacongo wenyewe! Kwa nini hawakupataifisha wakaibua mradi wa maana kama chuo, nk. Nachokiona katika wanaowalalamika sio kuwa wao wana mtazamo uliobora dhidi ya viongozi walalamikiwa bali wanaongozwa na chuki chuki chuki tu. Huo ndo uafrika.
 
Mobutu Sesseko Kuku ngendu Wazabanga baada ya kuingia madarakani kimabavu akaanza utawala wa kidikteta

Akajenga ikulu/kasri kubwa kijijini kwao Gbadolite ,akajenga uwanja mkubwa wa kutua ndege tena zilikua zile Concord ,uwanja huu alijenga kijijini kwao

Mobutu alipandisha hadhi kijiji cha kwao na kuwa jiji yani jiji la Gbadolite

Mobutu baada ya kufurumushwa madarakani kijiji kimebaki gofu malisho ya mbuzi na ng'ombe

Ikulu imabaki magofu na makazi ya popo

Uwanja wa ndege umebaki kutua ndege john na wengine walio umbwa na Mungu

Mobutu alikula sana hela za Nchi ya Zaire kujitajirisha na kujenga kwao

Leo hii kwao kumebaki magofu

Magufuli soma historia.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gbadolite
IkuluView attachment 1147267View attachment 1147269View attachment 1147270View attachment 1147271View attachment 1147272
Magufuli anadhani akitoka madarakani kina bashite na villaza wengine alio wateuwa watakuwa mabilionea hivyo watakuwa wanakwenda kumtembelea na private jet
 
Back
Top Bottom