Hapa tiptop barabarani Kuna chakula kitamu sana

Hapa tiptop barabarani Kuna chakula kitamu sana

Kuna sehemu nilikuwa nimeagiza msosi,sasa wakati nasubiri nikamuona mpakuzi kaenda na katoto kake kadogo kwa nje,kumbe kale katoto kanaharisha,yaani kabla hajakavua chupi vizuri kalimwaga UHARO kama Bomba la Dawasco [emoji134]Dada akakaacha kanaendelea kuhara akaingia ndani kuchukua jagi la maji mie namuangalia tu kisirisiri,akarudi nje akakatawaza bila hata sabuni,akarudi nako ndani akaenda kushika sahani aanze kupakua,nilikuwa na njaa lakini nilijifanya naongea na simu nikatoka nje,nilitoka nduki sikurudi tena!!hamu ya kula ilipotea siku nzima!!!mahali popote ukiona wahusika wapo na vitoto vyao vidogo ujue Usafi ni ZERO
Nimecheka sana hii[emoji23]

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Huwa nawaonea huruma sana watu wanaokula sehemu kama hizo, hata sijui kwanini!

Yani huwa nikiona walivyokaa wanakula, wengine wanasubiri nasikitika ila napata tumaini kwa kuona wamama wakiingiza kipato.
Upo kama mimi hata sijui kwanini nikiwaonaga moyo wangu unapata simanzi, kuna siku nilikuwa kituo kimoja cha daladala nikajikuta nimewazingatia sana mpaka najishangaa machozi yananitoka hata huwa sielewi ni nini kinafanya niumie
 
BRO ACHA KUTOA SIRI BANA
OK, HAPO TIPTOP MPAKA HAPA NJIA PANDA MABIBO.
VYAKULA VIZURI VIPO
 
Back
Top Bottom