Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Kwa Lugha ya picha ni kama watu mko safarini na ghafla gari mlilopanda likwame matopeni.
Haiyumkiniki nyie mlio garini wenyewe ndiyo muwe na uwezo wa kujikwamua toka matopeni mlipokwama.
Kama mnataka kujikwamua wenyewe hamna budi kushuka garini muingie matopeni msukume gari ili mtoke matopeni mlipokwama.
Njia ya pili ambayo ndiyo hutumika sana, ni kuwaomba watu walio nje ya Gari wawasukume mtoke matopeni mlipokwama. Njia hii inawafanya msichafuke Lakini Ina gharama.
Kama taifa ni kama sote tumo garini tumekwama matopeni. Njia ya kushuka tusukume wenyewe gari letu, hatuipendi. Na njia ya kutumia watu wengine watutoe hapa tulipokwama, nayo pia tunaogopa gharama zake.
Tumo tu garini tumekwama hatujui cha kufanya.