Uchaguzi 2020 Hapatoshi Singida Kaskazini, Nyalandu vs Ramadhani Ighondu

Uchaguzi 2020 Hapatoshi Singida Kaskazini, Nyalandu vs Ramadhani Ighondu

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Hili ni moja ya jimbo gumu sana upande wa CCM baada ya kinachosemekana kuwa ni makosa ya kamati kuu ya CCM kuwawekea mtu ambaye hafahamiki kabisa kushindanisha na Lazaro Nyalandu ambaye amekua kipenzi cha jamii ya watu wa eneo hilo.

Wenyeji wa ukanda huo wanasema Lazaro hatapata tu kura za Wanachadema pekee, bali ni hata WanaCCM ambao wanajua miaka yote kuwa yeye ndiye mbunge wao.

Huyu bwana Ramadhani Ighondo ambaye anatajwa kuwa ni mtumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu siyo mtu wa maneno sana isipokua ni mtu wa mikakati sana kiasi kwamba kumuelewa kwa kumtazama tu siyo rahisi.

Wanasingida Kaskazini twasubiri kipenga tuone mtanange huu. kikubwa refa awe fair na hata asipokuwa fair atashindwa kubeba mtu maana mbunge anajulikana mpaka sasa.

FB_IMG_15995923060595607.jpg
images-85.jpeg
 
Muuaji huyu hawezi kupata kura. Nyalandu kama vipi anialike hata mm nije nimsaidie kumpigia propaganda chafu dhidi ya huyu mgombea wa ccm (igondu).

Naweza hata nikavumisha kuwa huyu ndiye mkuu wa watu wasiojulikana walioongoza zoezi la kumpiga risasi kipenzi Cha watanzania Lisu, na wapiga kura wakaamini.
 
Inawezekana kabisa.
 
Wanasaikolojia wanasema ukitaka kumjua mtu na tabia yake au hata uwezo wa akili yake tazama viatu vyake anavyovaa au mavazi
Yaani ukisemea la viatu ndio kabisaa, angalia hizo raba za buku mbili mbili walizovaa
 
Back
Top Bottom