Hapendi nikose swala moja tu kwa siku, ananuna na kukasirika endapo nikikosa kufanya ibada

Hapendi nikose swala moja tu kwa siku, ananuna na kukasirika endapo nikikosa kufanya ibada

kiredio Jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2024
Posts
989
Reaction score
1,843
Habarini wadau

Yapata miezi kadhaa sasa tangu nipate mwenza, lakini ugomvi wake na mimi ni pale nitakapo acha kuswali swala moja tu kwa siku, hapo lazima nitoe maelezo na kununiwa.

Yeye ni mwanamke mwenye misingi ya dini na elimu ya dini ya Kiislamu, mimi pia ninafahamu lakini sio sana, lakini kupitia yeye najifunza mengi na kiukweli nimebadilika sana tangu nianzishe mahusiano na yeye. Alfajiri napigiwa simu kuamshwa kuswali na nafanya hivyo.

kituo kinacho fuata ni kuvuka maji au kutuma wawakilishi visiwani ikiwezekana nichukue jiko kwani naamini huyu ndiye mtu sahihi kwangu na kwa watoto wangu.

Nawahusia vijana wenzangu tutafute wanawake wenye maadili ya dini, haijalishi ni dini gani lakini yawe maadili ya kweli na siyo ya kuigiza.

Pia soma: Naombeni sifa za wanawake au mabinti kutoka Mafia
 
Hapaswi pia kukununia sababu ya wewe kutoshiriki ibada...

Anapaswa aombe Mungu mpaka ubadilike mwenyewe...
Kubadilika ni matakwa ya mtu wala sio Mungu.
NB: Sio kila anayesema Bwana Bwana ufalme wa Mungu atauona
Ni kweli lakini nimewasihi vijana wenzangu watafute wenza wenye imani za kweli wala sio wanaosema Bwana Bwana bila vitendo.....
 
Kubadilika ni matakwa ya mtu wala sio Mungu.

Ni kweli lakini nimewasihi vijana wenzangu watafute wenza wenye imani za kweli wala sio wanaosema Bwana Bwana bila vitendo.....

Kubadilika kiibada kunaanzia Rohoni kama umevutwa kimwili tu kuabudu lakini huna maandalio ya Roho ni sawa na kazi bure
 
Kubadilika kiibada kunaanzia Rohoni kama umevutwa kimwili tu kuabudu lakini huna maandalio ya Roho ni sawa na kazi bure
Kubadilika Kunaanzia Rohoni mwa mtu na sio Rohoni kwa Mungu..

Maamuzi ni ya mtu kwamba abadilike au La...
 
Je umetest mitambo au ndo mpaka ubani uchomwe?? Mkuu mwanamke wa kabla na baada ya ndoa ni watu wawili tofauti ishi nayo hiyo
Mkuu umesema kweli lakini bado naendelea kumsoma kila engo, ila kuhusu Tunda sidhani kama atakubali kabla ya ndoa.
 
Mkuu umesema kweli lakini bado naendelea kumsoma kila engo, ila kuhusu Tunda sidhani kama atakubali kabla ya ndoa.
Mna muda gani?? Na kama hatokubali ushawah muuliza kama ashawahi fanya au kuhimizwa kusali unaona malaika huyo

Mapichapicha mkuu stuka.
 
Back
Top Bottom