Hapi atema cheche Shinyanga "Tumejipanga kuhakikisha Dkt. Samia anapata ushindi wa sunami"

Hapi atema cheche Shinyanga "Tumejipanga kuhakikisha Dkt. Samia anapata ushindi wa sunami"

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Na Mwandishi Wetu

KATIBU MKUU WAZAZI ALLY HAPI AWATAKA VIONGOZI KUTOA USHIRIKIANO KWA MBUNGE KATAMBI.​

1737794674157.png

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ndugu. Ally Salum Hapi (MNEC) amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wajumbe wa mkutano mkuu kumpa ushirikiano wa kutosha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Ajira, Vijana na Walemavu) Mhe. Patrobas Katambi, pamoja na madiwani na viongozi wengine ili waendelee kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Agizo hilo amelitoa leo Tarehe 24/01/2025 kwenye mkutano mkuu wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini uliofanyika mjini hapa, akiwa mgeni rasmi wa mkutano huo, ambapo amewataka wajumbe wote kuwapa ushirikiano viongozi walioko madarakarani ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kuleta maendeleo, katika mkutano huo Katambi alisoma taarifa yake ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020 __ 2025.

"Niwaombe wajumbe wote wa mkutano mkuu mpeni nafasi ya kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa utulivu mbunge wenu ili aweze kitekeleza katika kipindi kilichobaki, kwani kuna baadhi ya watu wanatafuta watia nia, kumbe wanatengeneza mazingira ya kuvuta mpunga kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe, msipokuwa makini mtavurugwa, hivyo kuweni makini ndugu zangu, toeni ushirikiano ili aendelee kufanya maendeleo;

"Kuna baadhi ya wapambe feki tuachane nao, hivyo watia nia muwe makini, lengo langu lazima tuwape nafasi viongozi walioko madarakani kwanza ikifika wakati fomu zitatolewa watu watagombea sio sasa, tuzingatie maadili ya chama chetu" ameongeza.
1737794694924.png

"Katambi ameweza kutekeleza ilani ya CCM kuanzia pale alipochaguliwa mwaka 2020 kupitia chama chetu cha mapinduzi ambacho kilimpatia kazi ya kufanya hivyo kwa nafasi yake pamoja na madiwani na wenyeviti wametekeleza na wanatekeleza Ilani ya chama na chama kinasimamia serikali ili kuhakikisha maendeleo yanaonekana" amesema.

Hapi amesema Chama kinatarajia kuona wabunge madiwani na wenyeviti wanahudumia wananchi wote, kwa sababu wamechaguliwa ili watoe huduma za maendeleo si kusikiliza majungu ya watu.

"Nitoe rai kwa wabunge na madiwani kwamba huu mwaka uliobaki ni mwaka wa kutatua shida za wananchi tuwatembelee wananchi na kuhakikisha hiki kipindi kilichobaki tunatatua kero mbalimbali, na kazi lazima iendelee katika kipindi hiki" ameongeza.
1737794709462.png

Amesema Ilani isipotekelezwa chama cha mapinduzi ndicho kitakachoulizwa, sio mbunge au diwani, mtaji wa CCM ni kazi hivyo wasikwamishwe hawa viongozi, wakifanya hivyo watapata kura nyingi za kutosha kinachotakiwa wawe na umoja ndani ya Chama ili waweze kufanya makubwa zaidi na vikao vifanyike vya maendeleo sio vya maneno maneno tu ya kusemana.

"Niombe kamati zijadili mambo ya kuwasikiliza wananchi sio migogoro ya nyinyi kwa nyinyi kama kuna watu hawaelewani hapa na mmejaribu kuwapatanisha hawapatani waende wakayamalize wenyewe kuanzia sasa, kama wataendelea na ugomvi wao wakae pembeni kwanza wakiyamaliza ndiyo watarudi ni ni vizuri kuwapa misingi ya matumaini mazuri wananchi'' amesema Hapi.

Aidha amesema wanapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ni marufuku kiongozi yeyote kuenda kwenye kikao cha nje hajajiandaa, wawe na siasa zenye hoja na kila kata ijue nini kimefanyika cha maendeleo ili kukielezea na kila kiongozi wa kata awe na taarifa yake ya mafanikio.

"Nimepokea maombi ya mbunge kwa ajili ya barabara ya kwenda hospitali ya rufaa ya mkoa Mwawaza na mengine nitayafikisha huko ili kuhakikisha pale palipobakia panashughulikiwa, namjua Katambi ni mchapakazi, hivyo niwaombe madiwani shirikianeni nae" amesema Hapi.
1737794728956.png

"Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu tukumbuke kwamba uongozi unatoka kwa mungu pekee, eti wewe unasema una mgombea wako, mungu pekee ndiye anayejua nani kiongozi wa wakati huu na wakati ujao, tuwe na subira hata kama hujateuliwa kuwa na subira hukuandikiwa kuwa kiongozi kwa wakati huo, aliyeandikiwa kwa wakati huo ndiye atakayekuwa" alisema Hapi.
 
Back
Top Bottom