Hapo zamani za Kale – Hadithi kuhusu Afrika.

Hapo zamani za Kale – Hadithi kuhusu Afrika.

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Hapo zamani za Kale – Hadithi kuhusu Afrika.
Yaaminika bara la Afrika ndilo chimbuko la mwanadamu. Bara hili limekuwa makaazi ya falme nyingi na pia lililopoteza watu wake wengi kupitia biashara ya watumwa.

Hapo zamani za Kale – Hadithi kuhusu Afrika
4542519_803.jpeg

Yaaminika bara la Afrika ndilo chimbuko la mwanadamu. Bara hili limekuwa makaazi ya falme nyingi na pia lililopoteza watu wake wengi kupitia biashara ya watumwa.

Kwa upande mwengine tunaweza kusema asili ya mwanadamu ni Afrika. Hapa ndipo mwanadamu wa kwanza duniani yaamika aliishi. Miaka mingi baadaye, utawala wa kifalme ulianza kukita mizizi, kusambaa na hata kutukuzwa katika bara hili. Historia ya Afrika pia inatupa kumbukumbu ya nyakati za giza kama vile biashara ya watumwa, na utawala wa kikoloni uliotekelezwa na Wazungu.

Hebu sasa tuanze safari yetu kupekua historia ya Bara hili la Afrika na jinsi historia hii inavyochangia maisha ya sasa barani humu. Kama wasemavyo wahenga, “Ili kupata kujua unakokwenda ni lazima ujue unakotoka.”

Hata hivyo haya yasikujalishe kwani hayamo kwenye maandiko na kumbukumbu ya vitabu vya historia. Safari yetu kuhusu historia ya karne nyingi zilizopita barani Afrika, inazunguka katika maisha ya msichana mmoja kwa jina Julie, ambaye pamoja na bibi yake, wanafanya utafiti kuhusu historia ya bara hili.
 
Back
Top Bottom