Happy birthday AY : Mambo kumi usiyoyajua kuhusu yeye

GadoTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
370
Reaction score
636
1. Ni yeye ndiye aliyemfanya TID aanze kuimba. TID alikuwa rapper na mshereheshaji (MC). Girlfriend wa CBM Crew ndio wimbo waa kwanza kwa TID kuingia studio. “Wakati TID ana host show nakumbuka wakati ule Casey alikuwa ametoa wimbo wake ‘Missing You’, so kwakuwa TID alikuwa ni rapper na alikuwa ana host shows, alikuwa anauchombeza ule wimbo. Nilikuwa nikimsikiliza nasema ‘huyu jamaa anajua kuimba kwahiyo nikaenda naye kwa Master J.” 2. Alizaliwa Shangani, Mtwara, July 5, 1982.

3. Ameishi kwenye mikoa mingi na Dodoma alikuwa akiishi mtaa mmoja na akina Mangwair. “Tumecheza wote, nilikuwa nawafundisha table tennis, roller-skates.” 4. Aliwahi kuingia fainali kwenye mashindano ya Umiseta kwa kucheza table tennis. Fainali zilifanyika Arusha.

5. Alianza kusoma darasa la kwanza kwenye shule ya Msingi Mwembeni ya Musoma, Mara.

6. Kundi lake la kwanza la hip hop liliitwa ‘Two Problem’ akiwa na Swedi na Aluta
7. Aliandaa show yake ya kwanza kama promoter akiwa kidato cha pili. “Niliandaa show nikawaleta GWM, wakati huo wanapiga ‘Cheza Mbali na Kasheshe’, halafu unawatoa watu Dar unawaleta Dodoma, unawalipia nauli nini, nakumbuka alikuja KR na Inspekta Haroun.”
8. Wimbo wake wa kwanza kuingia studio unaitwa Kipi Kikusikitishacho

9. Alihamia kutoka Morogoro kuja Dar kutafuta maisha na hakuwa na ndugu. “Nilikuwa nakaa kwa washkaji, nilikuwa nakaa kwa akina Buff G na kwingine. Chumba changu cha kwanza kupanga kilikuwa Magomeni.
10. TV yake ya kwanza kuinunua bado ipo. “Mpaka leo inawaka, haijawahi kuharibika hadi leo.”

Chanzo: Chill na Sky. Unaweza kusikiliza kipindi hicho cha redio kwa kuclick link kwenye bio ya skytanzania
 
Last edited by a moderator:

sasa hivi mziki umemshinda,kabaki kuwa dalali wa kazi,mfano mzuri ni alivyomfanyia udalali domo(kaya) kwa davido
 
Last edited by a moderator:
Pia leo diamond platnumz amethibitisha kua AY ndie aliyeshiriki kumuunganisha na Davido mpaka wakatoa single!Na pia ndie aliyemuunganisha na Godfather.

Nimezidi kumuheshimu sana leo AY,hakika huyu ndie mfalme wa bongofleva hapa bongo,sikujua kama ana moyo wa kipekee wa kusaidia watu kiasi hiki.Mungu aendelee kumbariki siku zote
 
Happy birthday Ambwene hakika umeitendea haki tasnia ya bongo fleva
 
sasa hivi mziki umemshinda,kabaki kuwa dalali wa kazi,mfano mzuri ni alivyomfanyia udalali domo(kaya) kwa davido

Muziki haujamshinda, wimbo wake wa 'Zigo' unafanya vizuri. Problem ni kwamba watu sasa hivi kipimo cha mtu kufanya vizuri imekuwa Diamond which is very wrong. Diamond yupo level yake anawazidi ata manguli wengi wa Africa.

Nashauri tusianze kutusi ata awa legends ,kuwatusi wakongwe ni kuwakatisha tamaa wasanii wachanga coz ata awa tunaowapenda sasa baadae watakuwa wakongwe, tukiwaheshimu wakongwe tunawapa moyo vijana wa sasa kina diamond kiba vanessa kufanya mambo wanayojua yataacha kumbukumbu nzuri.
 

Pengine huyu leo amevunja record ya kupostiwa kwenye mitandao...
 
Hakika amevunja record!Yaani leo birthday yake imekuwa ya furaha na heshima kubwa!kweli huyu kaka anapendwa

Kweli huyu jamaa ana kubalika maana hadi nimeshangazwa.. Nifuraha na inatia moyo kuona watu wana thamini mchango wako tena ukiwa hai..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…