Kimbley
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 3,050
- 2,104
Hongera AY kwa kujianzishia thread. Swali.
Video ya zigo lini?
Ukipewa ban hapa utasema umeonewa!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hongera AY kwa kujianzishia thread. Swali.
Video ya zigo lini?
sasa hivi mziki umemshinda,kabaki kuwa dalali wa kazi,mfano mzuri ni alivyomfanyia udalali domo(kaya) kwa davido
Pia leo diamond platnumz amethibitisha kua AY ndie aliyeshiriki kumuunganisha na Davido mpaka wakatoa single!Na pia ndie aliyemuunganisha na Godfather.
Nimezidi kumuheshimu sana leo AY,hakika huyu ndie mfalme wa bongofleva hapa bongo,sikujua kama ana moyo wa kipekee wa kusaidia watu kiasi hiki.Mungu aendelee kumbariki siku zote
Mkuu yaani AY ni msanii anayejitambua sana, hana makuu, hana mibifu ya kijingajinga. Hana wivu kwa wasanii wanaofanya vizuri kwenye game, yeye kwa lolote ambalo liko ndani ya uwezo wake anakuaidia vizuri sana.
Nakumbuka ndiye msanii wa kwanza kuanza kupasua anga za Kimataifa kwa kufanya kazi na wasanii wa nje. Alianza kiutani tu kwa kufanya kazi na CMB Prezzo pale Kenya na wimbo wao Nipe nikupe ulihit sana enzi hizo na mpaka leo huchoki kuusikia, toka hapo akapasua zaidi mpaka kufanya kazi zi Kingston si mchezo.
Nakumbuka yeye na MwanaFa ndiowaliokuwa wasanii wa mwishomwisho kuachana na kundi la GK (Nimesahau jina) Wasanii wote walikimbia na kuanza kufanya mziki kama solo lakini wao walikomaa hata baada ya Gk mwenyewe kuanza kuchuja walibaki mpaka walipoona sasa basi. Kumbuka Wasanii walikuwa wakifanya vizuri kwenye kundi hilo ni yeye na MwanaFa tu GK kwenyewe alikuwa haoni ndani kwa hao jamaa. Kwakweli Mungu amzidishie sana AY
Unaikumbuka ngoma ya HII LEO
BACK TANGANYIKA
Ukipewa ban hapa utasema umeonewa!
Pia leo diamond platnumz amethibitisha kua AY ndie aliyeshiriki kumuunganisha na Davido mpaka wakatoa single!Na pia ndie aliyemuunganisha na Godfather.
Nimezidi kumuheshimu sana leo AY,hakika huyu ndie mfalme wa bongofleva hapa bongo,sikujua kama ana moyo wa kipekee wa kusaidia watu kiasi hiki.Mungu aendelee kumbariki siku zote
Then watu wanasema ni management ya Daimond ndo iko vizuri
Iko vizuri my a.ss!
kila kitu kinamchango wake ndugu.... kumbuka collable ya kwanza ya kimataifa ni nakupenda by iyanya...
Hata hivyo ommydimpoz alipewa pande akamshirikisha jmartins kwanini hayupo alipo diamond???
unaufahamu wimbo wa pallaso ft. davido umetoka mwaka huu lakini pallaso anahit??
Radio na weasel walitoa wimbo wao na wizkid lakini je wapo alipo diamond hivi leo???
Mwisho tu, heshima yake sana AY huyu jamaa kwangu mimi ndio true legend kwa wanamuziki ninaowafahamu Afrika mashariki, hustle zake ni zaidi ya diamond ila tu diamond amejua zaidi mikakati, management ipo poa na nyota..
Happy birthday AY
Ni ammikiki wa kipindi cha MKASI akishirikiana na Salama Jabir
Nilikusubir usahau kusema nyota nikukumbushe.
Unajua ukimfatilia Naseeb (Dai) toka anatoka hakuna cha ajabu saaana alichokifanya tofauti na wenzie akina belle9 na wengine wengi.
Hii tunzo ya msanii chipukiz alopewa baraka ingekuwa kapewa Diamond ungeona mripuko wake.
Kuba wasanii weng wagen kwenye industry mf. Ruby,Sam,malaika,mirror,mo music n.k lakn kuna unaemwona anaonesha dalili za kuwa Diamond?
Wanadai inshu ni kudate na Wema,vip akina Jumbe,Charles Baba,bayser (inasemekana),include huyo bwana mpya (Linah tingz) vp wao mbona hawajawa Diamond kwenye kaz zao??
Kwa sis tunaoamini kuna kitu kinaitwa "kupakwa mafuta" ndo hicho nnachokiona kwa Diamond.Nan anamkumbuka Cpwaa? Si alitoa sana video sauz? Then?
Mwisho kabisa,namnukuu FA "Mungu hakupi kama hataki,na hata....." Mwisho wa kunukuu.
Hongera AY kwa kujianzishia thread. Swali.
Video ya zigo lini?
1. Ni yeye ndiye aliyemfanya TID aanze kuimba. TID alikuwa rapper na mshereheshaji (MC). Girlfriend wa CBM Crew ndio wimbo waa kwanza kwa TID kuingia studio. Wakati TID ana host show nakumbuka wakati ule Casey alikuwa ametoa wimbo wake Missing You, so kwakuwa TID alikuwa ni rapper na alikuwa ana host shows, alikuwa anauchombeza ule wimbo. Nilikuwa nikimsikiliza nasema huyu jamaa anajua kuimba kwahiyo nikaenda naye kwa Master J. 2. Alizaliwa Shangani, Mtwara, July 5, 1982.
3. Ameishi kwenye mikoa mingi na Dodoma alikuwa akiishi mtaa mmoja na akina Mangwair. Tumecheza wote, nilikuwa nawafundisha table tennis, roller-skates. 4. Aliwahi kuingia fainali kwenye mashindano ya Umiseta kwa kucheza table tennis. Fainali zilifanyika Arusha.
5. Alianza kusoma darasa la kwanza kwenye shule ya Msingi Mwembeni ya Musoma, Mara.
6. Kundi lake la kwanza la hip hop liliitwa Two Problem akiwa na Swedi na Aluta
7. Aliandaa show yake ya kwanza kama promoter akiwa kidato cha pili. Niliandaa show nikawaleta GWM, wakati huo wanapiga Cheza Mbali na Kasheshe, halafu unawatoa watu Dar unawaleta Dodoma, unawalipia nauli nini, nakumbuka alikuja KR na Inspekta Haroun.
8. Wimbo wake wa kwanza kuingia studio unaitwa Kipi Kikusikitishacho
9. Alihamia kutoka Morogoro kuja Dar kutafuta maisha na hakuwa na ndugu. Nilikuwa nakaa kwa washkaji, nilikuwa nakaa kwa akina Buff G na kwingine. Chumba changu cha kwanza kupanga kilikuwa Magomeni.
10. TV yake ya kwanza kuinunua bado ipo. Mpaka leo inawaka, haijawahi kuharibika hadi leo.
Chanzo: Chill na Sky. Unaweza kusikiliza kipindi hicho cha redio kwa kuclick link kwenye bio ya skytanzania
muziki haujamshinda, wimbo wake wa 'zigo' unafanya vizuri. Problem ni kwamba watu sasa hivi kipimo cha mtu kufanya vizuri imekuwa diamond which is very wrong. Diamond yupo level yake anawazidi ata manguli wengi wa africa.
Nashauri tusianze kutusi ata awa legends ,kuwatusi wakongwe ni kuwakatisha tamaa wasanii wachanga coz ata awa tunaowapenda sasa baadae watakuwa wakongwe, tukiwaheshimu wakongwe tunawapa moyo vijana wa sasa kina diamond kiba vanessa kufanya mambo wanayojua yataacha kumbukumbu nzuri.
We Kweli tundu kunuka!sasa hivi mziki umemshinda,kabaki kuwa dalali wa kazi,mfano mzuri ni alivyomfanyia udalali domo(kaya) kwa davido
hilo la pili la mwaka wake wa kuzaliwa ni uongo!!! AY hajazaliwa 1982.