Daaah..! Kweli vyuma vimekaza..! Yaani mpaka kikwete leo anaonekana mtu mzuri..! Huyu ndo rais aliyetukanwa zaidi kuliko marais wote waliopita na hata huyu wa sasa...
yaani we acha tu!!
nakumbuka alipokuja obama mhariri wa tanzania daima, ngurumo, ambaye kwa hakika alikuwa anamchukia mno kikwete.....licha ya kuponda meeengi sana kwa makusudi kabisa kuhusu ziara hiyo, alifikia hatua ya kuandika hivi, ''obama anasapoti ushoga, hivi ikulu yetu itabaki salama?....akikosekana raisi vipi salma hatopatikana?''. hivi ndivyo alivyoandika mhariri huyu.....ni dharau na matusi ya kiwango cha juu kiasi gani haya!!!!! lakini mzee yule wa msoga licha ya kuwa na uwezo wa hata kumuoa kabisa huyu ngurumo, alimaliza muda wake bila ya kumdhuru kwa namna yoyote ile.....nafikiri ngurumo atakutana na matusi yake siku ya hukumu!
tulipokuwa na mgogoro wa kimipaka na malawi, ngurumo tena akaandika mengi kuwa raisi haijui mipaka ya nchi yake.......alipokuja kutoa hotuba mwenyewe, kila mwenye akili alielewa.
sijasahau na yale maandishi makubwa yaliyoandikwa katikati ya barabara ya rami pale dar, ''KIKWETE NCHI IMEKUSHINDA''.
sijazungumza kuhusu zomeazomea ya pale UDSM,....kuitwa dhaifu hadi mat.shirt yakachapishwa,....kuitwa mujahidinan.k.
leo hii anakumbukwa hiviiii, kweli watz wengi ni wanafiki sana aisee!!!!