Hongera ya Kuzaliwa Mange!
Wewe ndio sauti ya watanzania kwa sasa. Pale vyama viliponyamazishwa umetumia nafasi yako kuongelea wengi. Pale vyama vilipokosea umetumia nafasi yako kuvikaripia. Kwa sasa wewe ndio mkombozi, sauti mbadala wa ile ya serekali. Umeifanya vyema kazi ya kuisimamia serekali kwa kuelimisha, kuibua na kuchunguza mienendo ya serekali. Twaweza tusikubaliane kila jambo ila vita unaipiga vema. Pole kwa kuwa uhamishoni ila najua iko siku historia itakukumbuka.
Siasa tunazoshuhudia kwako ni kama mpira wa Pele. Unafanya maadui na wapenzi wako kutaka kujua nini unachokuja nacho. Maadui zako wanakupenda sema hawawezi kukiri tu. Nakutakia kila la kheri kwenye maisha yako. Mungu akubariki