Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,649
- 4,786
Mnamo tarehe 21 ya mwezi wa 3 mwaka 1980 hukoo Porto Alegre nchini Brazil, alizaliwa mtume na nabii wa mwisho wa Soka.
Ujio wake ulitarajiwa, kwani ishara nyingi zilishajionesha kuwa mbarikiwa atakaekuja kutambulisha skills zinazopatikana katika ligi haswa ya Mbinguni yu karibu kuzaliwa.
Kuzaliwa na kukua kwake kulikuwa ni kwa kibinaadamu zaidi na alisoma na kupata malezi kama watoto wengine mpaka alipotimiza miaka 13 ndipo matendo ya kinabii yakaanza onekana.
Akiwa na umri huo Dinho aliisaidia timu yake ya mtaa kupata ushindi wa goli 23-0 magoli ambayo yote aliyatupia yeye.
Huyu ndie Ronaldo de Assis Moreirra almaarufu kama Ronaldinho Gaucho the saint ambae akiwa uwanjani basi Malaika huacha shughuli zao na kuanza kumtazama.