Happy Birthday Sakayo

Mungu ni mwema, ni mwaminifu sana kwangu!
Namshukuru kwa umri mpya alonijaalia, wazazi, ndugu, kazi, pumzi na akili!

Lakini zaidi namshukuru Mungu kwa kunipa marafiki ambao wamekuwa kama ndugu, wana JF nyie ni kama ndugu zangu! Namshukuru Mungu sana kwa hilo!

Nitakuwa mnafiki kushukuru Mungu bila kuwaombeni msamaha nyinyi ndugu zangu, najua wapo niliowakwaza kwa kujua ama kutokujua! Sababu Biblia inatuasa tuitafute kwanza amani na watu woote, naomba niwaombe mnisamehe pale nilipowakwaza ama kuwaumiza kwa namna moja ama nyingine!

Mkinisamehe naamini na sala zangu za shukrani zitapokelewa!

Niwashukuru mnoo, wanafamilia wangu wa jf kwa kuwa na mimi, mnanifanya nacheka hata nikiwa chumbani peke yangu! .
Dada Shunie pokea shukrani zangu!


Kutoka ndani ya sakafu ya moyo wangu, NAWAPENDA sana, yaaani sana!!

N.B: Zawadi napokea mwenyewe jamani kwa namba zile zile za voda![emoji7][emoji7][emoji8]
 
MITHALI 14:1-2 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba, Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe, yeye aendaye kwa unyofu wake humcha Bwana bali aliye mkaidi ktk njia zake humdharau [emoji120][emoji120]

salaaaam insta babe...

happybirthday sakayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…