Marahabaaa......
Nimesubiri weeee nione nani atajipendekeza lakini hola! Imekula kwangu mazima.
Anyway nimetoka mbali wakulu
Katoto katundu....
Kijana mtukutu, mbunifu, mkaguzi na asiyependa kupitwa na jambo...
Kijana rijali mwenye mhemko wa kibaiolojia, mabinti hawakukatiza kirahisi....
Mzee wa makamo anayeenda na wakati.....
Mzee Brazamen anayejichanganya kitaa.....
Na Sasa...........Mzee mtu mzima aliyeamua kutulia.....
Bado maisha yanasonga mbele!!
Ahsante Mungu kwa kuniweka hai mpaka leo, kunijalia afya tele na maisha ambayo najisikia amani duniani.
Ahsante Mama kwa kunizaa, kunilea na kunitunza kwenye maadili mema.
Ahsante Baba kwa kumuoa mama, na kumpa nafasi na uwezo wa kufanya yote aliyonitendea huku ukiwa kioo cha maisha yangu.
Ahsante mke wangu kwa kukubali kuolewa na mimi na kuishi na mimi kwa mapenzi ya hali ya juu (shenzy zao waliokuwa wakikumendea ukawapiga chini)
Ahsante wanangu kwa kuwa watoto wazuri, kuheshimu wazazi ndugu jamaa na marafiki na kuwa mfano bora kwa watoto wenzenu. (Sijawahi juta kuwa baba yenu)
Ahsante walimu wangu, wallah bila chaki zenu ningekuwa mkulima stadi aliyechoka mbaya
Ahsante TBL, SBL, TDL, Grants, kwa kuhakikisha maisha yangu yanakuwa ya burudani tele na ubongo wangu kuwa na utulivu
Ahsante Condoms (Hapa sina cha kusema zaidi, dongo lingeshanifukia siku nyiiingi)
Ahsante mabaamedi.... anyway.
Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, Ahsante JF members hasa CC na MMU kwa kunifanya niwe na marafiki wa ukwee waliopatikana kwa uwezo wa vidole vyangu...
Kwa watakaokuwa na nafasi, tafrija ya shukrani itafanyika Etiennes Bar, Boko Basihaya Kaunta ya Juu.
Wanajamii kumi watakaofika wa kwanza watapata bia tatu baridi za bure na wataruhusiwa kujichagulia mhudumu wa kuwahudumia.
Mungu awabariki sana, na karibuni nyote katika safari ya kulijongelea kaburi.