Happy Birthday to Me! OMG!!!ODM anazidi kulisogelea kaburi...

Happy Birthday to Me! OMG!!!ODM anazidi kulisogelea kaburi...

Binti neggirl, ukibofya ID yangu na kuseslekti opsheni ya Praiveti Meseji, utanikuta nakusubiri kwenye Inbox ya PM zangu. hebu do the needful ili niamini kweli we ni mtoto mzuri.

hihi hihiiiiiiiiii... babuuuuuu Asprin here I come stay tuned.
 
Last edited by a moderator:
Thanks hommie. Lakini hebu angalia tarehe uliyopost hii makitu na tarehe ya thread mama.....:becky::becky: Nshaanza kunywa biya mwenzio LOL

Am waiting......... Eagerly!:mwaaah::mwaaah::mwaaah:

Kwa hali ilvyo bora uendelee kumsubiri neggirl hommie....thats the way to go maana kama umeshaanza kunywa bia lazma na kikojoleo kinafanya kazi yake mujarab
 
Last edited by a moderator:
Marahabaaa......

Nimesubiri weeee nione nani atajipendekeza lakini hola! Imekula kwangu mazima.

Anyway nimetoka mbali wakulu

Katoto katundu....

attachment.php



Kijana mtukutu, mbunifu, mkaguzi na asiyependa kupitwa na jambo...
528555_315247641878196_1998471866_n.jpg


Kijana rijali mwenye mhemko wa kibaiolojia, mabinti hawakukatiza kirahisi....

attachment.php


Mzee wa makamo anayeenda na wakati.....

attachment.php


Mzee Brazamen anayejichanganya kitaa.....

attachment.php



Na Sasa...........Mzee mtu mzima aliyeamua kutulia.....

attachment.php



Bado maisha yanasonga mbele!!

Ahsante Mungu kwa kuniweka hai mpaka leo, kunijalia afya tele na maisha ambayo najisikia amani duniani.
Ahsante Mama kwa kunizaa, kunilea na kunitunza kwenye maadili mema.
Ahsante Baba kwa kumuoa mama, na kumpa nafasi na uwezo wa kufanya yote aliyonitendea huku ukiwa kioo cha maisha yangu.
Ahsante mke wangu kwa kukubali kuolewa na mimi na kuishi na mimi kwa mapenzi ya hali ya juu (shenzy zao waliokuwa wakikumendea ukawapiga chini)
Ahsante wanangu kwa kuwa watoto wazuri, kuheshimu wazazi ndugu jamaa na marafiki na kuwa mfano bora kwa watoto wenzenu. (Sijawahi juta kuwa baba yenu)
Ahsante walimu wangu, wallah bila chaki zenu ningekuwa mkulima stadi aliyechoka mbaya
Ahsante TBL, SBL, TDL, Grants, kwa kuhakikisha maisha yangu yanakuwa ya burudani tele na ubongo wangu kuwa na utulivu
Ahsante Condoms (Hapa sina cha kusema zaidi, dongo lingeshanifukia siku nyiiingi)
Ahsante mabaamedi.... anyway.

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, Ahsante JF members hasa CC na MMU kwa kunifanya niwe na marafiki wa ukwee waliopatikana kwa uwezo wa vidole vyangu...

Kwa watakaokuwa na nafasi, tafrija ya shukrani itafanyika Etiennes Bar, Boko Basihaya Kaunta ya Juu.
Wanajamii kumi watakaofika wa kwanza watapata bia tatu baridi za bure na wataruhusiwa kujichagulia mhudumu wa kuwahudumia.

Mungu awabariki sana, na karibuni nyote katika safari ya kulijongelea kaburi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Weee jamaaa wewe
 
Back
Top Bottom