Nimeuliza siku ya sabato kuwa jumamosi nionyeshwe kwenye Biblia neno Jumamosi lilipo sijaulliza maana ya sabato usinilishe maneno
Hujaniuliza mimi, lakini naomba nisaidie kujibu swali lako.
Neno jumamosi limeandikwa mahali pengi sana ndani ya Biblia. Ukiona sehemu pameandikwa neno
sabato basi jua imemaanishwa neno jumamosi.
Kwa nini nasema hivyo.
Sababu
Neno sabato ni neno la kiitalia liwakilishalo siku ya saturday katika kiingereza, na waitalia waliyohoa kutoka kwenye neno sabbatum ambalo ni neno la kilatini.
"Sabato" is the Italian word for "Saturday." It comes from the Latin "sabbatum," which means the Sabbath, a day of rest in many religious traditions.
Kwenye Biblia ya Kiswahili cha kisasa (iliyoandikwa na padri wa kule jimbo la Tabora), neno jumamosi limetajwa katika kitabu cha Matendo 20:7.
Matendo 20:7 BHN
[7] Jumamosi jioni tulikutana ili kumega mkate. Kwa vile Paulo alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliwahutubia watu na kuendelea kuongea nao hadi usiku wa manane.
Twende sasa kwa nini sabato ndiyo iwe siku ya kuabudu.
Kama wewe ni mkristo, bila shaka unaamini Yesu alikufa msalabani. Na bila shaka unajua alikufa ijumaa (biblia ya kimvita imetumia neno maandalio ya sabato)
Yohana 19:31
[31]Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe.
The Jews therefore, because it was the preparation, that the bodies should not remain upon the cross on the sabbath day, (for that sabbath day was an high day,) besought Pilate that their legs might be broken, and that they might be taken away.
Siku ya sabato (jumamosi) Yesu alikuwa kaburini, bila shaka unaamini kuwa Yesu alifufuka siku ya jumapili (ambayo hata leo huazimishwa kama siku ya kufufuka kwa Yesu katika kile kinaitwa Pasaka).
Sasa, siku ya kufufuka kwa Yesu Kristo, Biblia ya kiswahili cha kimvita huiita SIKU YA KWANZA YA JUMA, lakini katika Biblia ya kiswahili cha kisasa huiita Jumapili.
Nakuletea mafungu hayo nikiianza na mistari toka kiswahili cha Kimvita, kisha mistari hiyo hiyo, nitaileta kwa kiswahili cha kisasa.
KISWAHILI CHA KIMVITA
Yohana 20:1
[1]Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
The first day of the week cometh Mary Magdalene early, when it was yet dark, unto the sepulchre, and seeth the stone taken away from the sepulchre.
Mathayo 28:1
[1]Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
In the end of the sabbath, as it began to dawn toward the first day of the week, came Mary Magdalene and the other Mary to see the sepulchre.
KISWAHILI CHA KISASA
Yohane 20:1 BHN
[1] Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.
Mathayo 28:1 BHN
[1] Baada ya Sabato, karibu na mapambazuko ya siku ile ya Jumapili, Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikwenda kutazama lile kaburi.
BNH huwakilisha Biblia Habari Njema.
Mimi nakamilisha hivyo mchango wangu, endeleeni na mabishano yenu.