Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,606
- 1,711
- Thread starter
- #21
Tanzania yenye neema bila mdhaifu na mwoga companero inawezekana. Kabebe maboksi mkuu, tuachie nchi yetu watanganyika.
Ewe Mtanganyika jasiri usiye dhaifu wala mwoga nchi yenu Watanganyika ilishazikwa zamani ndio kaburi lake linafukuliwa na madini yake yanapokwa kila kukicha - Hebu msikilize mzikaji wake akijibu hii hoja yenu majasiri:
"Vijana wa Tanganyika hawana haja ya kumbembeleza ye yote wala chombo cho chote kuhusu utaifa wao; wanalijua Taifa lao. Si jingine ni Tanganyika. Tanzania ife, izikwe, ioze. Hatuitaki"
Mimi nawaheshimu kwa dhati kabisa vijana waliotoa kauli hii. Nawaheshimu kwa sababu wana akili, wana ukweli, na wana ujasiri. Wana akili za kutosha kutambua kuwa ukifufua Tanganyika, Tanzania itakufa; wana ukweli unaowazuia kutumia hila za maneno matupu kama "ndani ya Muungano," kudanganya watu wadhanie kuwa unaweza kuwa na serikali ya Tanganyika, na bado Tanzania ikabaki...Lakini Tanganyika haitasaidia chochote. Hizi jitihada za kututoa kwenye haja ya kutazama kwa makini sababu halisi za matatizo ya nchi yetu, ili tuseme kuwa sababu za matatizo yetu ni Tanzania, na dawa yake ni Tanganyika, ni jitihada za kunywesha watu kasumba.
- Julius K. Nyerere, Tanzania! Tanzania!