Harakati Sasa Basi - Narudi Kubeba Maboksi!

Harakati Sasa Basi - Narudi Kubeba Maboksi!

Tanzania yenye neema bila mdhaifu na mwoga companero inawezekana. Kabebe maboksi mkuu, tuachie nchi yetu watanganyika.

Ewe Mtanganyika jasiri usiye dhaifu wala mwoga nchi yenu Watanganyika ilishazikwa zamani ndio kaburi lake linafukuliwa na madini yake yanapokwa kila kukicha - Hebu msikilize mzikaji wake akijibu hii hoja yenu majasiri:

"Vijana wa Tanganyika hawana haja ya kumbembeleza ye yote wala chombo cho chote kuhusu utaifa wao; wanalijua Taifa lao. Si jingine ni Tanganyika. Tanzania ife, izikwe, ioze. Hatuitaki"

Mimi nawaheshimu kwa dhati kabisa vijana waliotoa kauli hii. Nawaheshimu kwa sababu wana akili, wana ukweli, na wana ujasiri. Wana akili za kutosha kutambua kuwa ukifufua Tanganyika, Tanzania itakufa; wana ukweli unaowazuia kutumia hila za maneno matupu kama "ndani ya Muungano," kudanganya watu wadhanie kuwa unaweza kuwa na serikali ya Tanganyika, na bado Tanzania ikabaki...Lakini Tanganyika haitasaidia chochote. Hizi jitihada za kututoa kwenye haja ya kutazama kwa makini sababu halisi za matatizo ya nchi yetu, ili tuseme kuwa sababu za matatizo yetu ni Tanzania, na dawa yake ni Tanganyika, ni jitihada za kunywesha watu kasumba.

- Julius K. Nyerere, Tanzania! Tanzania!
 
Process is more important than outcome. When the outcome drives the process we will only ever go to where we've already been. Stagnation and eventually throw in the towel. If process drives outcome we may not know where we're going, but we will know we want to be there. We will have the will power to never stop no matter what.

Mwanaharakati wa kweli Che alikuwa na mwili dhaifu sana lakini mambo aliyoyafanya tunayazungumza leo na yataendelea kuzungumzwa vizazi vingi vijavyo.

....Natumai nitatumia muda huo kutafakari ni wapi nilikosea katika harakati zangu za kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania. Kama nitapata jibu, basi labda nitajipanga upya na kurudi tena kujiunga na wanaharakati kujaribu kuendeleza taifa hili. Kwa sasa roho inataka ila mwili ni dhaifu.....

Wanao na wajukuu wako hawatakuelewa hapo. Hii vita tunayopigana sasa watakaofaidi matunda yake sio sisi bali ni vizazi vijavyo. Miaka mitano kwenye uliongo wa mapambano katika Tanzania ya leo ni midogo sana. Hawa tunaopigana nao wamejichimbia very deeply and greenly.

Aluta continua....
 
Process is more important than outcome. When the outcome drives the process we will only ever go to where we've already been. Stagnation and eventually throw in the towel. If process drives outcome we may not know where we're going, but we will know we want to be there. We will have the will power to never stop no matter what.

Mwanaharakati wa kweli Che alikuwa na mwili dhaifu sana lakini mambo aliyoyafanya tunayazungumza leo na yataendelea kuzungumzwa vizazi vingi vijavyo.

Wanao na wajukuu wako hawatakuelewa hapo. Hii vita tunayopigana sasa watakaofaidi matunda yake sio sisi bali ni vizazi vijavyo. Miaka mitano kwenye uliongo wa mapambano katika Tanzania ya leo ni midogo sana. Hawa tunaopigana nao wamejichimbia very deeply and greenly.

Aluta continua....

Impact mkuu, impact, where is the impact of this process of harakati? Giza la Tanesco? Sumu ya Dawasco?
 
Basi hata JK tusimlaumu, miaka 5 haimtoshi. Tumuongezea 5 mingine.
Sawa sawa, aidha kwa upande wako licha ya kutoweka wazi namna ulivyoendesha harakati zako na namna ulivyoshindwa, unakaribishwa tena kubeba maboksi....

Hiari yashinda utumwa
 
Mwanaharakati wa kweli huwa hachoki daima

Ni kweli uyasemayo, ila kumbuka pia kuwa wakati wa mapambano kondoo anaporudi nyuma si kwamba kachoka au kaogopa bali anakusanya nguvu ili arudi na shambulio kubwa na lenye impact kubwa kuliko lile la awali.

Mwache akabebe maboksi huenda atakaporudi atakuwa mwanaharakati bora kuliko alivyokuwa hapo kabla
 
Mkuu shairi lako zuri (sehemu ya pili). Linasema yaliyoyakweli. Kwenda kubeba maboksi si kitu kibaya as long umeona kuwa by doing so utakaporudi utaweza kubadili kiti. Lakini kama unakwenda kubeba maboksi kwa kuwa tu umechoka baada ya kujariba harakati zikagoma hapa. Maboksi hata hapa yanabebwa mbona si lazima uende mbali. ILA HARAKATI NI POPOTE. PAMBANA MKUU UKO UENDAKO KUBEBA MABOKSI. UTUKUMBUKE KWA KUTURUSHIA JAPO KABOKSI KAMOJA KAMOJA.
 
Nchi imejaa neema, tumia akili utafanikiwa
Acha kulalama bure, unataka nchi ikupe nini?
Mwanaharakati kuharakati nini, Unapumbazwa na JF
Mwenye busara huifanyia nchi, siyo nchi iwafanyie kazi!
Nenda kabebe Boksi, hiyo ni qualification yako!
 
Hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii hapa nchini inazidi kuwa tete, hii ikiwa ni miaka 5 toka nirejee kwa moyo wote kuja kujenga Taifa. Pamoja na harakati zote hizo bado hali ya umaskini inadhidi kukithiri. Ufa kati ya matajiri na maskini wa Bongo inazidi kuongezeka. Rasilimali zetu zinazidi kuporwa. Na nchi imeingia gizani kama ilivyotabiriwa na wadau wa umeme.

Sasa nimeamua kurudi kubeba maboksi. Natumai nitatumia muda huo kutafakari ni wapi nilikosea katika harakati zangu za kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania. Kama nitapata jibu, basi labda nitajipanga upya na kurudi tena kujiunga na wanaharakati kujaribu kuendeleza taifa hili. Kwa sasa roho inataka ila mwili ni dhaifu. Naam, nia ya kubaki na kuvumilia ninayo, sababu ya kubaki na kuvumilia ninayo, ila uwezo wa kubaki na kuvumilia sina.

*Wapi maboksi yanabebeka kwa tija na elimu nzuri ya maendeleo inapatikana?

Companero,

Pole sana kiongozi; heri wewe una kwa kukimbilia, sisi walalahoi hatuna kwa kukimbilia kuikwepa hii jehanamu.

Sisi hapa tukipata nafasi ya kwenda nje ni kufika Malawi ambako nako siku hizi wanaonja joto la watawala wao ambao wengi ni kutoka Tanzania (Wakimbizi walioshi TZ muda mrefu).

Kama unaweza nenda kabebe boksi na pumzisha akili lakini rudi na nguvu mpya na mikakati mipya.

Sisi wengine ni Ngangari na tutabanana hapa hapa.
 
Hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii hapa nchini inazidi kuwa tete, hii ikiwa ni miaka 5 toka nirejee kwa moyo wote kuja kujenga Taifa. Pamoja na harakati zote hizo bado hali ya umaskini inadhidi kukithiri. Ufa kati ya matajiri na maskini wa Bongo inazidi kuongezeka. Rasilimali zetu zinazidi kuporwa. Na nchi imeingia gizani kama ilivyotabiriwa na wadau wa umeme.

Sasa nimeamua kurudi kubeba maboksi. Natumai nitatumia muda huo kutafakari ni wapi nilikosea katika harakati zangu za kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania. Kama nitapata jibu, basi labda nitajipanga upya na kurudi tena kujiunga na wanaharakati kujaribu kuendeleza taifa hili. Kwa sasa roho inataka ila mwili ni dhaifu. Naam, nia ya kubaki na kuvumilia ninayo, sababu ya kubaki na kuvumilia ninayo, ila uwezo wa kubaki na kuvumilia sina.

*Wapi maboksi yanabebeka kwa tija na elimu nzuri ya maendeleo inapatikana?

Winners never quit bro.
 
Nchi imejaa neema, tumia akili utafanikiwa
Acha kulalama bure, unataka nchi ikupe nini?
Mwanaharakati kuharakati nini, Unapumbazwa na JF
Mwenye busara huifanyia nchi, siyo nchi iwafanyie kazi!
Nenda kabebe Boksi, hiyo ni qualification yako!
Neema neema gani, ufisadi waita wema
Kuharakati ndio nini, huko kuganga njaa
Maboksi yangu fani, wataka niwe papaa
Kama huwezi kughani, sikiza ya malenga:

Lipi likusumbualo, kalamu kuirukia
Au umekosa mlo, sasa umechukia
Lipi hasa ulonalo, unalolisumbukia
Kama shida ni uhuru, tushapata 61

Amani tulonayo, ni tunu ilotufikia
Usitake mapambano, shimoni tatumbukia
Sijeichokoza leo, kesho hutoifikia,
Kama shida ni uhuru, tushapata 61

Jaribu kujipa moyo, manani takusikia
Kuwa mtu wa maono, lengo utalifikia
Siwachukie vigogo, nchi wameitumikia
Kama shida ni uhuru, tushaupata 61

Siwatafute wanono, waweza kukuchukia
Mwisho wakakutoa roho, bure kwa kujitakia
Ogopa sana vigogo, chini watakufukia
Kama shida ni uhuru, tushaupata 61

Wale uwapiganiao, kesho watakukimbia,
Hawatoshiriki mgomo, Wala kukuimbia,
Tena watakaa kando, huku wakijitambia,
Kama shida ni uhuru, tushaupata 61

We kula ugali wako, ukishiba tajitapikia,
Achana na nia yako, wengine kuhangaikia,
We jali maisha yako, wenye shida wajitakia,
Kama shida ni uhuru, tushaupata 61

Chukua hatua zako, uone utapoangukia,
usitafute maneno, balaa likakufikia,
Mwombe sana Mola wako, 'mana' takushukia,
Kama shida ni uhuru, tushaupata 61

Kama hawapendi jambo, hawawezistahimilia,
Madhari wanapata tango, shida wanavumilia,
Siku wakikabwa shingo, mabosi watasimulia
Kama shida ni uhuru, tushaupata 61

Shida zikiwakaba koo, watajua pa kukimbilia
Tena watafanya soo, mabosi watajililia,
Patakuwa ni padogo, mawe yatasimulia,
Kama shida ni 61, uhuru tushaupata?

© Ayub. R.
 
Acheni ushabiki usiokuwa na tija. 48years of freedom mmepambana na nini na mmejivunia nini kama si kurudi nyuma hatua mia?... Nakuunga mkono Mkuu Companero, we nenda huko ulikopanga kwenda, riziki ni popote bana.Hawa wanaokukatisha tamaa wana nasaba na ufisadi...wanafaidika hawa!Nenda mwana-kwenda, usiangalie nyuma!
 
Wewe nenda ufike salama uendako,
Sisi wengine tunaendeleza mafao,
Uhuru umeshapatikana uamuzi ni wako,
Tanzania kuna neema kwa wenye macho.
Kikwete kaweka wazi wananchi katoa fursa
Hana ubaguzi wala kinyongo ni wewe fanya mambo,
Rudi kabebe boksi hiyo ndiyo fani yako.
 
Tanzania itajengwa na wenye MOYO na italiwa na wenye CHOYO
 
Wewe nenda ufike salama uendako,
Sisi wengine tunaendeleza mafao,
Uhuru umeshapatikana uamuzi ni wako,
Tanzania kuna neema kwa wenye macho.
Kikwete kaweka wazi wananchi katoa fursa
Hana ubaguzi wala kinyongo ni wewe fanya mambo,
Rudi kabebe boksi hiyo ndiyo fani yako.

Uhuru wake bendera, huo ndio utumwa
Rais wetu ombaomba, nasi wananchi pia
Uchumi huo twakalia,mafisadi hao jichumia
Kezaji nalo latucheka, madini yetu lachota
 
Uhuru wake bendera, huo ndio utumwa
Rais wetu ombaomba, nasi wananchi pia
Uchumi huo twakalia,mafisadi hao jichumia
Kezaji nalo latucheka, madini yetu lachota
Uhuru tunao uchumi tunao,
Ufisadi tabia miongoni tunao,
Mahakama wapo sasa wanashughulika

Muulize Yona MrambaLiyumba habari hiyo
Usimsahau mgonja huo ndiyo mwisho wao
Ubaya kuufanyia watu malipo ndiyo hayo
Rais anahangaika kuwatumikia wananchi
Kutembea kuitangaza nchi tufaidi wote
Madini twapata mrahaba dunia ndiyo hivyo

Nenda kabebe boksi hiyo ndiyo fani yako
Umebaki kulalama hakuna jema unaloona
umekuwa kipofu kiziwi wakujitakia
sisi tunachukua fursa twendeleza nchi
nenda sala uendako uhuru ni wako.
 
Nani kakwambia nchi maskini, wabongo vibanda wachimbia ardhini,
Anzia tegeta hadi kibaha, kila mtu A/c kujiachia ndani ya mchuma,
Zunguka river side hadi msimbazi, vikao vya harusi vyalindima,
Hadi kimbilia kubeba maboksi, nani kakwambia wabongo maskini?
 
Tanzania itajengwa na wenye moyo inaliwa na wenye meno
Kazi kwenu Kila leo tunadanganywa eti uchumi umekuwa kule Ufipa hakuna hata barabara wale walioiona ile filamu ya FIMBO YA MNYONGE basi tosha kwa nchi hii
 
we campanero kabebe zako boksi,wala mtu asikutishe
 
Back
Top Bottom