ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
Cliton Revocatus Chipando a.k.a Baba Levo wa kwanza kutoka kushoto enzi za ubarobaro wake, picha ya kwanza akiwa kijana mdogo kabisa, picha inayofuata akiwa kwenye show na kundi lake la OBD & GAZ akiwemo Kijukuu Zero Sifuriii ooh, huyu Kijukuu Zero Sifuri Ooh, alikuwa ni bingwa sana wa mashairi au michano kwa lugha tata.
Hii ilikuwa ni mwaka 2003 katika ukumbi wa Cine Atlas Makondeko Ujiji, Baba levo alikuwa anatamba na wimbo wake wa Mapadri na Mashee
Clayton chipando alikuja akawa Diwani wa kata ya mwanga 2015-2020 kupitia chama cha ACT -Wazalendo.
Kigoma ilibarikiwa kuwa na wasanii wengi enzi hizo, na makundi mengi ya wasanii yaliundwa Kigoma ikiwemo kundi la ''Red spider'' kutoka Ujiji na kina Baba Levo walikuwa wakitokea Mwanaga.
Makundi mengi ya Ujiji yalisambaratika baada ya msanii wao mkubwa kutanganza kuacha muziki na kufariki siku chache mbeleni, huyu alikuwa ''Fad Moh'', alikuwa mwenye kipawa na talanta ya hali ya juu katika uimbaji na mipangilio ya sauti ya maghani. Ukiachana na Koffi Olomide katika kubadilisha ladha ya sauti pia ''Fad Moh'' alikuwa ni bingwa wa kubadili sauti kwenye Mic.
Miaka hiyo kulikwa na wasanii wa aina zote hapa kwetu Kigoma, hata midundo ya singeli ilianzia huku na iliendeshwa na mwamba 'Ali Sinina' na mauno.
Kigoma kulikuwa na wasanii wengi kama kina gado brain siwasikii, walikuwepo kina Igwee na pah one, tupo around na masela ni kolabo na kidman, ilisifika k.town RFA hewani, usiku uligeuka raha, chege chigunda mtoto wa mama saidi kwa kasim zaid hawa walikuwa Mwazimwi kutoka Ujiji kisha wakajiita Manyema Family, kwa kuwamiss kundi la change dollar-mambo hadharani, raha ikageuka shida, tambo la obd na gaz na wake mrembo, Iddi Nyundo a.k.a Chamjicho. Ujiji walimmiss Jasmin, r.i.p fad moe, lilo kilio kwa mtaa, mitoto ileee na leader walisema game bado, bring kuhit na mchumba, wapi subwenke ya zinja, grem na vuga wana dumba, Nagasaki pembe za chaki, kwenye mic hawakubaki, hizo zilikuwa fataki, zilizotamba na kuwika hapa kwetu Kigoma Ujiji. Hizi ni kumbukizi za burudani, mapumziko ya weekend, bangwe beach watu walispend, heshima kwa Kid, Hitman na Maximum Record.
Picha ya mwisho aliyevalia miwani na kupiga salut ni Malilo au Lilo Boy alikuwa rafiki kipenzi wa Marehemu 'Fad Moh'. (Mwasu)
Ukwaju wa kitambo
#funguka.
K town people fungukeni mtueleze kigoma kunani???