Harakati za Ben Saanane kupambana na Rais Magufuli, ni njia sahihi ya kuwaridhisha wafadhili wake?

Hivi kuna mtu au kiongozi ambaye yupo perfect?? Kukosolewa ni kuambiwa kwamba hauko perfect kwahiyo ni kawaida
 
Nimesoma Tuu jina lako hapo juu kukuta Ni ww sisomi Uzi wako maanake najua Ni kada wa chama
 
Tehetehetehetehe. Mbona sisi huwa tunasoma utumbo mnaoandika? Utafanyaje uchambuzi kama hujasoma?
 
Mkuu ameona kikosi chenu hakina uwezo wa kupambana, ndiyo maana ameamua kuoeleka maombi yake kwa Malaika.
Waulize akina Slaa, Michael Aweda, Zitto Kabwe, Samson Mwigamba, Kitila Mkumbo, Henry Kilewo, Lema na wengineo ambao tulipambana nao kwa hoja. Sasa umebaki ujinga tu wa akina Ben Saanane
 
Mwanzoni mwa mwaka huu, niliweka taarifa kwenye mitandao ya kijamii hususan hapa Jamiiforums juu ya Mkuu wa Sera na Utafiti CHADEMA, Ben Saanane kununuliwa vitendea kazi kama simu, kompyuta mpakato, ipad, tablets na zana nyingine. Nilieleza kuwa aliyemnunulia vitu hivyo ni Edward Lowasa. Nilitoa sababu za Lowasa kufanya hivyo ni kutaka Mkuu huyo wa Sera na Utafiti afanye kazi ya kumsafisha Lowasa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia amshambulie Rais Magufuli ili tunapoingia 2020, asiaminike tena. Nilieleza kuwa Ben na Lowasa wamekubaliana kuwa malipo ya kazi hiyo ni milioni 4 kwa mwezi.

Kwenye uzi ule, nilieleza bayana kuwa Ben Saanane amepangiwa ofisi ya kufanyia kazi hiyo katika sehemu ambapo sikubainisha kwenye mtandao kutokana na sababu za kimkakati.

Hata hivyo, baada ya uzi ule kuwekwa, Ben Saanane alikosa uvumilivu. Aliishia kuporomosha lugha zilizokosa staha kwa lengo la kushinikiza mods waufute. Alifanikiwa. Uzi ule ukaenda na maji. Leo mdogo wangu Ben namuomba awe mvumilivu ili tujadili kwa staha.

Miezi 5 imepita sasa tangu Ben Saanane anunuliwe. Matunda ya uwekezaji ule yameanza kuonekana. Ben Saanane na genge lake wameanza mashambulizi dhidi ya Rais kwa hoja ambazo kimsingi hazina mashiko.

Ben Saanane na genge lake wameshindwa kabisa kuona udhaifu wa Rais Magufuli kiutendaji na badala yake wanaegemea kwenye mipasho na mapambio. Wanafanya siasa za kuvizia. Niliwahi kuanzisha mada humu kwamba, ikitokea Rais akawa bubu, je CHADEMA watakuwa na ajenda zipi?

Tathmini yangu ya muda mfupi imebaini kwamba, hoja zinazojengwa na Ben Saanane na genge lake zinategemea nini Rais anaongea. Kwa maana utendaji wa Rais uliotukuka unasababisha Ben Saanane na Genge lake wakose hoja za kumkosoa. Hata kama wanapojaribu kukosoa utendaji, wanakosoa kwa hoja dhaifu. Mathalan, ziliponunuliwa ndege mpya mbili aina ya Bombadier Q400, walijenga hoja za kitoto eti ndege hizo hazina mwendo. Mara wanasema ni mapangaboi. Mara wanasema eti water salute haikufanyika kisawasawa. Almradi wanawaonesha wafadhili wao kuwa wametimiza wajibu wao. Utoto.

Uwezo wa vijana wa CHADEMA katika kujenga hoja ni mdogo. Kuna wakati Lusinde aliwahi kuwaambia kuwa akili zao zimeshikiliwa na Mbowe na ndio maana wanawaza kimbowembowe tu.

Hata hivyo, najaribu kuwaza, je kazi anayofanya Ben Saanane na genge lake inatosheleza matakwa ya wafadhili wake? Je watafanikiwa kushusha morali ya Rais Magufuli katika kuwatumikia wananchi? Je watakwamisha juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Magufuli katika kutekeleza ilani ya CCM? Thubutu! Rais ameapa kuwa hakuna atakayekwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM. Ben Saanane na Genge lake wataishia kujadili water salute, kuomba Salary Slip ya Rais na kujipongeza kutokana na kauli ya Rais kuwa anatamani malaika afungie mitandao ya kijamii kwa mwaka mmoja ili itakapofunguliwa wakute Tanzania imepaa.

Nimhakikishie Rais wangu kuwa, hawa wapiga kelele mitandaoni hawatafanikiwa kukwamisha harakati zako za kuwaletea maendeleo wananchi. Waache wapige kelele. Wewe piga kazi. Mwisho wa siku kelele zao zitageuka kuwa kicheko kwako. Watanzania tuna imani kubwa kwako. Kazi unayofanya inapokelewa kwa mikono miwili na Watanzania. Utafiti wa Twaweza unabainisha kuwa 96% ya Watanzania wanakulibali. Endelea kupiga kazi ili ifikapo 2020, wapinzani waone aibu kumsimamisha mgombea Urais kupambana na wewe.

Ni sahihi kabisa!! hamna haja ya kujibizana na mtu Wa tabia za yuda Iscariot!! Rais wetu apige Kazi Mungu Wa mbingu na nchi yuko pamoja naye!! Watapambana lakini hawatashinda!!!
 
Vijana wana njaa Kali. wanatumika wanapata pesa za makombo.
Huyo jamaa ukute elimu yake ni ya kuunga unga kama ya Mbowe & Co.
 
kweli nyani hajioni kundule! yaani hata wewe umesahau kitengo chako hapo Lumumba cha kumponda lowassa?! au Ben kakuzidi maujanja!? acha hizo bwana!
 
Umechemka kidigo, Chadema imekodishwa na ma Mvi kwaiyo mwa miaka yote aliyo kodi yeye anaendelea kua mgombea wa Urais. DJ ataendelea kua Mwenyekiti wa Chama.
 
Aya ni mambo ya aibu pale saa 8 anapo lamba viatu vya ma Mvi ili aendelee kuishi. Ni zaidi ya Unyumbu.
 
Waulize akina Slaa, Michael Aweda, Zitto Kabwe, Samson Mwigamba, Kitila Mkumbo, Henry Kilewo, Lema na wengineo ambao tulipambana nao kwa hoja. Sasa umebaki ujinga tu wa akina Ben Saanane
Pamoja na yote, safari hii imekuwaje hadi mkuu atake msaada wa Malaika?
 
"Siasa siyo sayansi halisi" anasema Bismark wa Ujerumani katika hotuba yake kwenye Prussia Chamber tarehe 18.12.1863. Alikuwa sahihi.
=====
imetafisiriwa hisivyo rasmi kutoka andishi la Mh. P. Msekwa kwenye gazeti la Daily News la 29.09.2016 ukurasa wa 7
 
Mwanzoni mwa mwaka huu, niliweka taarifa kwenye mitandao ya kijamii hususan hapa Jamiiforums juu ya Mkuu wa Sera na Utafiti CHADEMA, Ben Saanane kununuliwa vitendea kazi kama simu, kompyuta mpakato, ipad, tablets na zana nyingine. Nilieleza kuwa aliyemnunulia vitu hivyo ni Edward Lowasa. Nilitoa sababu za Lowasa kufanya hivyo ni kutaka Mkuu huyo wa Sera na Utafiti afanye kazi ya kumsafisha Lowasa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia amshambulie Rais Magufuli ili tunapoingia 2020, asiaminike tena. Nilieleza kuwa Ben na Lowasa wamekubaliana kuwa malipo ya kazi hiyo ni milioni 4 kwa mwezi.

Kwenye uzi ule, nilieleza bayana kuwa Ben Saanane amepangiwa ofisi ya kufanyia kazi hiyo katika sehemu ambapo sikubainisha kwenye mtandao kutokana na sababu za kimkakati.

Hata hivyo, baada ya uzi ule kuwekwa, Ben Saanane alikosa uvumilivu. Aliishia kuporomosha lugha zilizokosa staha kwa lengo la kushinikiza mods waufute. Alifanikiwa. Uzi ule ukaenda na maji. Leo mdogo wangu Ben namuomba awe mvumilivu ili tujadili kwa staha.

Miezi 5 imepita sasa tangu Ben Saanane anunuliwe. Matunda ya uwekezaji ule yameanza kuonekana. Ben Saanane na genge lake wameanza mashambulizi dhidi ya Rais kwa hoja ambazo kimsingi hazina mashiko.

Ben Saanane na genge lake wameshindwa kabisa kuona udhaifu wa Rais Magufuli kiutendaji na badala yake wanaegemea kwenye mipasho na mapambio. Wanafanya siasa za kuvizia. Niliwahi kuanzisha mada humu kwamba, ikitokea Rais akawa bubu, je CHADEMA watakuwa na ajenda zipi?

Tathmini yangu ya muda mfupi imebaini kwamba, hoja zinazojengwa na Ben Saanane na genge lake zinategemea nini Rais anaongea. Kwa maana utendaji wa Rais uliotukuka unasababisha Ben Saanane na Genge lake wakose hoja za kumkosoa. Hata kama wanapojaribu kukosoa utendaji, wanakosoa kwa hoja dhaifu. Mathalan, ziliponunuliwa ndege mpya mbili aina ya Bombadier Q400, walijenga hoja za kitoto eti ndege hizo hazina mwendo. Mara wanasema ni mapangaboi. Mara wanasema eti water salute haikufanyika kisawasawa. Almradi wanawaonesha wafadhili wao kuwa wametimiza wajibu wao. Utoto.

Uwezo wa vijana wa CHADEMA katika kujenga hoja ni mdogo. Kuna wakati Lusinde aliwahi kuwaambia kuwa akili zao zimeshikiliwa na Mbowe na ndio maana wanawaza kimbowembowe tu.

Hata hivyo, najaribu kuwaza, je kazi anayofanya Ben Saanane na genge lake inatosheleza matakwa ya wafadhili wake? Je watafanikiwa kushusha morali ya Rais Magufuli katika kuwatumikia wananchi? Je watakwamisha juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Magufuli katika kutekeleza ilani ya CCM? Thubutu! Rais ameapa kuwa hakuna atakayekwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM. Ben Saanane na Genge lake wataishia kujadili water salute, kuomba Salary Slip ya Rais na kujipongeza kutokana na kauli ya Rais kuwa anatamani malaika afungie mitandao ya kijamii kwa mwaka mmoja ili itakapofunguliwa wakute Tanzania imepaa.

Nimhakikishie Rais wangu kuwa, hawa wapiga kelele mitandaoni hawatafanikiwa kukwamisha harakati zako za kuwaletea maendeleo wananchi. Waache wapige kelele. Wewe piga kazi. Mwisho wa siku kelele zao zitageuka kuwa kicheko kwako. Watanzania tuna imani kubwa kwako. Kazi unayofanya inapokelewa kwa mikono miwili na Watanzania. Utafiti wa Twaweza unabainisha kuwa 96% ya Watanzania wanakulibali. Endelea kupiga kazi ili ifikapo 2020, wapinzani waone aibu kumsimamisha mgombea Urais kupambana na wewe.
Anza na TWAWEZA
 
Naona lizabon na ww umeajiriwa kupambana na CCM kubambana na Ben,hasa kipindi hichi ambacho nafasa za Ukurugenz zko waz kule kagera...Lkn hio nafas huipati kwa kuwa huk mitandaoni tu umegalagazwa....Nataman malaika washuke waifunge mitandao y kijamiii
 
Back
Top Bottom