Ukweli unauma bila shaka. Ukisikia Manchester United imeenda Korea Kusini kwa ajili ya Pre season, basi ujue lengo kubwa hapo ni kwenda kuongeza idadi ya mashabiki na kufanya biashara, ikiwemo ya jezi!
Sasa ukiulizwa ulazima wa Pre season ya simba Misri! Utajibu nini? Kuna Mmisri atashawishika kweli kuwa mshabiki wa simba, badala ya Al Ahly, Zamaleki, nk!!! Na kama ni suala tu la utulivu, basi nchi yetu imejaliwa maeneo mengi yenye utulivu! Likiwemo lile eneo la Avic Town kule Kigamboni!
Au ni ushamba tu na ulimbukeni!