Harakati za kuacha Umalaya Zilivyogonga mwamba baada ya ndoa

Harakati za kuacha Umalaya Zilivyogonga mwamba baada ya ndoa

Huo ni ugonjwa mkuu...😂😂😂.
 
Kukunja hela na kumshikisha wakati wa kupeana Amani haiwezekani kwa sababu baada ya kumaliza kwako atamoa mkono mtu mwingine..labda kama ungesema ulimvizia nje ndo ukampa namba ila hii umetupiga fix ya wazi
Hata mie niliona kuwa ametupiga chai. Na sijui alipokuwa anaandika numba ya simu kwenye hiyo hela alikuwa kanisani ndani au aliandaa toka nyumbani. Fix nyingine akawapige watoto wa sekondari
 
Wenzangu wapendwa!

Kufanya umalaya sio Jambo jema Ila kwa mwanaume nimegundua kuacha Umalaya Ni kazi ngumu sana kuliko wake zetu wanavyotufikilia.

Mwanzo nilidhani labda kwa sababu ya siendi kanisani ndiyo maana nikawa Malaya vile!
Ikabidi nianze kwenda kanisani ibada ya pili! Mwanzoni nikaona kiasi ilinisaidia, lakini benchi nilipokuwa kuwa nikikaa kila jumapili Kuna mlimbwende nae alipenda kuja kukaa eneo lile!

Nilipata Wakati mgumu Sana kusikiliza mahubiri lakini nilikomaa hivyohivyo, Kwenye kipengele Cha kutakiana amani bwana (wakatoliki wanaelewa), Ikabidi yule mrembo nimkunjie mkono elf 5 na number ya simu!
Baada ya missa nikiwa gheto enzi hizo, yule binti alinitafta! sikuchelewesha tukafanya yetu!

lakini mle kanisani kulikuwa na binti mwingine ambaye yeye nilimuona akijibinua Sana hasa Wakati wa kutoa sadaka! nikapita nae vilevile!

kiukweli sikupenda tabia ile lakini ilitokea tu!

Baada ya kusali kwa miezi kadhaa, mmoja akanishawishi niingie kuimba kwaya ya Vijana!
Aisee huko ndo kabisa sauti ya kwanza nikawala wote na wakagombana Sana na kwaya nikaacha!

Ikabidi Hadi kanisani nianze kukaa nje, maana ndani huko niliona aibu kabisa kuingia.

Nikaamua kumfuata Padre anisaidie! of course alifanikiwa kunishauri kuliko kuwaka tamaa Bora nione!
Nikafanikiwa kuchagua mmoja!

Kimbembe Ni pale ndoa ilipotangazwa kanisani! yaani hizo meseji nilizopokea huko inbox usiombe! ..baadhi wengine walinisonya na wengine waliita" Wee Mbwaa kabisa Malaya mkubwa, ..wengine walitumia kiingereza "Ur a lier! n.k
wengine waliendelea kunipa mzigo hivyo hivyo na ndoa ikiwa imetangazwa!
Siku ya ndoa waimba kwaya jicho walilonipiga hakika mke wangu laiti angejua ndoa ingevunjika siku ileile!

Iliniwia vigumu Sana kuhudhuria iventi au mikusanyiko mkubwa na wife maana lazima tu nitakutana na X -girlfriend!

Iwe beach au matamasha au Banda la abiria ilinibidi nivae miwani mieusi na kapero ili angalau niwe na Aman kuepusha shali!
Kiufupi Umalaya ulinikosesha raha kabisa!
Nilivyokuwa kwenye ndoa kidogoo Mambo yalipungua lakini mke wangu alivyopata Mimba akawa kisirani!

Hapo ndipo mtihani ukaanza tena! Sikuzoea kukaa wiki bila kufanya mapenzi!
mke alipojifungua ndo kabisaa kisubiri siku arobaini ikawa Ni shida kubwa Sana! Nikaendelea kuchepuka!

Kiufupi nikiwa kwende ndoa nilipunguza kasi lakini nimeshindwa kabisa kabisa kuacha kugonga inje!

Kuna Wakati nasimamisha usiku na mke wangu akiwa pembeni kitandani lakini hamu Ile inakuwa ya kutaka uchi mpya!
Nampenda mke wangu lakini haka kaujinga kakuchepuka ni upuuzi wangu tu ambao nataman Sana kuuacha Ila ndo nimeshindwa!
Nawaza hata kubadili dini niwe mwisilam ili nioe wake watatu angalau nikiwa kwa huyu nimkumbuke yule na yule!
Lakini bado nimepitia Sheria ya ndoa inasema Ni mke wa kwanza anahaki ya kutoa pingamizi ndoa isifungwe!

Sheria ya ndoa inanibana ili niweze kuongeza mke lazima ndoa ya awali iwe na msingi wa dini ya wake wengi!

NIPO KWENYE HARAKATI ZA KUACHA UMALAYA LAKINI BADO NI CHANGAMOTO SANA!
Kwahiyo mwamba ndio tushakupoteza.
Daaah

#YNWA
 
Hata mie niliona kuwa ametupiga chai. Na sijui alipokuwa anaandika numba ya simu kwenye hiyo hela alikuwa kanisani ndani au aliandaa toka nyumbani. Fix nyingine akawapige watoto wa sekondari
Brother ukisoma utaelewa yule dem nilikuwa namuwinda dhana zote niliandaa! Mbona hijaniuliza ile pesa nilipatawapi nikampa
 
Sio ww tu tupo wengi sana mdogo wangu sema wengi wetu humu ni wanafiki wataonyesha kukushangaa while they are the one who do to the fullest even more than you.
 
Sio ww tu tupo wengi sana mdogo wangu sema wengi wetu humu ni wanafiki wataonyesha kukushangaa while they are the one who do to the fullest even more than you.
Ni ngumu sana hata cjui ilikuwaje
 
Back
Top Bottom