Harakati za msanii Mack Dizzo kwenye game ya bongo fleva

Harakati za msanii Mack Dizzo kwenye game ya bongo fleva

Respect kwa kazi zako. Nyimbo yako ya Shuga Mummy, ilikuw pini kali

Una ugomvi na unique sisters?
 
1. Kifo cha nyani
2. By show

Zinanikumbusha miaka hiyooo
 
Zamani kabla Chuo cha Muhimbili (MUHAS ya sasa) hakijajitegemea kilikuwa kikiitwa Muhimbili University College of Health Sciences (MUCHS) ambayo ilikuwa college chini ya UDSM.
Sawa. Hapo nimekusoma.
 
HARAKATI KAMILI ZA MACK DIZZO & UGLY FACES KWENYE GAME YA BONGO FLEVA KABLA YA CHID BENZ KUITAWALA "ILALA"

kiukweli mimi kama mack dizzo ni mtoto wa ilala pure kabisa...

Harakati na mishe zangu zote nimefanyia ilala since way back in 1990s..

" kwa kifupi ilala ndio my home street " harakati zangu zote nimefanya nikitokea ama nikiwa nakaa ilala..

sisi wasanii wa zamani tulikuwa tunashiriki kwenye matamasha & corcept mbalimbali zilizoandaliwa mashuleni Enzi hizo kwenye maeneo mbalimbali kama vile jitengemee..

Kundi letu la mwanzo kabisa Enzi hizo mimi kama mack dizzo kujiunga nalo lilikuwa linaitwa " ugly faces"
Miaka ya 1996/7

Ni crew ambalo liliundwa na wasanii watatu (3) ambapo ni mimi mack dizzo, Easy dazz & rich mack ambaye kwa sasa yupo Marekani kama dj kwa sasa pamoja na Easy Dazz kwahiyo kibongo bongo nikawa nimebaki mimi.

Ndipo nikafanya maamuzi na nikaanza kufight kwenye Game ya Bongo fleva nikiwa kama solo Artist nje ya crew ..

Shindano la C.b.m ambapo kirefu chake ni " check Bob maarifa" shindano ambalo liliandaliwa na Designer mmoja hivi ..

Katika competition hiyo mimi nilikuwa kama mshindi wa kwanza na washindi wa pili walikuwa ni crew ya S.O.G "( space of Gangsters)

Crew ambayo alikuwepo wasanii kama Ay , snare , Buff G .

Mimi kama mack dizzo nilishika nafasi ya kwanza (1) katika lile shindano .

Na wao kama Crew ya S.O.G " ( space of Gangsters) walishika nafasi ya Pili (2) katika lile shindano..

Pale baada ya shindano hilo kukamilika yule designer aliamua kuwachukua kabisa kwahyo

Ay , snare & buff G wakaamua kujiita ( C.b.m crew) check Bob maarifa..

Yule designer aliwachukua maana aliwakubali sana Enzi hizo ..

Kwenye upande wa ile "Hip hop halisi Decomentary ilifanyika katika ukumbi mmoja hivi mitaa ya kinondoni karibu kabisa na kijiwe kimoja maarufu sana Enzi hizo " American chips.

Ukumbi huo ulikuwa unaitwa " FM CLUB" ..

Ambapo Enzi hizo sisi tukiwa bado wadogo palikuwa panaitwa " lang'ata"

Kulikuwepo na wasanii na producer wengi Tu kama vile p funk majani , solo thang , snaz Tee, soggy doggy & Bad G ( witness a.k.a kibonge mwepesi)

Na wengine wengi..

Sisi "ugly faces" ndio ilikuwa Crew pekee inayowakilisha mtaa wa Ilala wote Enzi hizo kulikuwa hakuna crew nyingine zaidi ya " ugly faces"

Mpaka pale washkaji zangu waliposafiri wakaenda zao America ..

Baada ya hapo ndio wakapatikana wasanii wengine kama Dully sykes , Chid benz ..

Lakini "ugly faces" ndio tulikuwa waanzirishi wa movement za Muziki ilala Enzi hizo..

Baada ya harakati za hapa na pale kama solo Artist ndipo nikaja kukutana na msanii anaitwa " Godfrey Tumaini a.k . Dudu baya tukaanzisha kitu kinaitwa " Da skendo" kiukweli "Da skendo " lilikuwa sio kundi kama wengi walivyodhani hapo awali miaka ile ya nyuma wakati mimi nipo na Dudu baya..

Sisi tulienda kwenye Tamasha Moja la wasanii Zanzibar Enzi hizo .
sasa kwa miaka ile ya nyuma wasanii wengi ambao walienda kushiriki lile Tamasha ..

walikuwa ni Aina fulani ya wasanii ambao hawataki kuonekana mara kwa mara street , sehemu mbalimbali za starehe nyani kwa kifupi muda mwingi walikuwa ni watu wakujifungia ndani na kutokupenda kuonekana mbele za watu kabla ya Tamasha kufanyika huko Zanzibar...

Kwahiyo Kati ya hao wasanii mimi na Dudu Baya tukajikuta daily leo tunaingia Club hii kesho Club nyingine na maeneo mbalimbali ya starehe huko Zanzibar hata iwe usiku wa manane ilikuwa ni mwendo wa party after party..

Urafiki wangu mimi na Dudu Baya ndio Chachu iliyopelekea kuanzishwa kwa " Da skendo"

Da ilisimama kama kifupi cha neno ama jina " Dar es Salaam na Neno " skendo " lilisimama kama vituko ama matukio ..
Kwenye miaka 2005/6..

Yote hii ilipelekea kujiita "Da skendo" ni kutokana na mapito yetu Enzi hizo mimi na Dudu Baya , watu wa matukio mara hivi mara vile nyani ilikuwa ni hatari...

Watoto wa mjini tunaweza

kusema " wazee wa skendo za town"

Makundi ya mwanzo kabisa yaliotuinspire sisi ni kama vile " The demplowmatz" , kwanza Unit, Hard blastaz nk .

Kwa Taifa la Marekani watu kama kina lil Cool jay , produce r kama Dr. Dre ndio walituinspire..

Nyimbo yangu ya " Sugar mumy" niliyomshirikisha Msanii Dully sykes Enzi hizo ni True Stori ambayo ilimtokea jamaa yangu wa karibu sana ambaye tulikuwa nae katika Crew yetu ya " ugly faces"

Anaitwa "Eazy Dazz" yenye ndio alikuwa anaishi maisha hayo kama messenge ama ujumbe unavyosema katika ile Ngoma .

Alikuwa anaishi na Girlfriend wake ambae alikuwa anasoma University of Dar Es Salaam anasomea mambo ya udoctor na alikuwa anajimama lilikuwa linafanya Kazi pale kwenye ofisi za T.R.A ..

Kwahiyo jamaa akawa anachukua fedha kutoka kwa yule mama mfanyakazi wa T.R.A na kwenda kuenjoy na yule Girlfriend wake...

Kwahiyo Hii ni True stori jambo hili liliendelea mpaka pale jamaa alipoamua kusafiri kwenda zake Marekani Enzi hizo. .

Kabla hajasafiri jamaa yangu aliweza kuisikia ile Ngoma ya " Sugar Mumy " na kusema Da jamaa yangu , mbona message ama lycris zilizopo Humu ni kama umeniimbia mimi wimbo ho..

Nikamueleza hamna msela wangu hii ni kama sanaa tu ..

Kwahiyo kwa namna Moja ama nyingine maisha ya msela wangu wa karibu yakawa yamenipa Ngoma na mpaka leo hiyo Ngoma kali..

🔥🔥🔥🔥

Changamoto niliyoipata ni ile dhana au Desturi ya wazee wetu Enzi hizo kuwa kijana anayefanya Muziki ni muhuni tu ..

Unaonekana umepoteza Dira katika Maisha na hutaki shule, ndio changamoto kubwa ambayo tulikuwa tunaiface sisi kama wasanii Enzi hizo..

Kipindi nakutana na msanii Dudu Baya alikuwa Tayari ana hit songs kama vile " mwanangu huna nidhamu, na alikuwa na kundi ama crew yake inaitwa " Dudu Baya Foundation"

Ndio walikuwepo wale madogo kama Dogo hamidu nk ..

Da skendo alikuwa kundi in search ilikuwa kama tu utambulisho ukiniona mimi kwenye stage na Dudu Baya ujue ni " Da skendo" ila sio crew kama wengi wanavyofahamu..

Dudu Baya na mimi kila mmoja alikuwa ana project zake binafsi kama solo Artist..

Muunganiko wangu mimi na Dudu Baya ulikuwa unapatikana pale lilipotokea ama kualikwa kwenye Tamasha kwenda kuparform pamoja..

Kiukweli hatukubahatika kufanya Kazi ya pamoja kama " Da skendo" ingawa na kumbukumbu kuna wimbo mmoja ulijulikana kwa jina la " Baba mwenye nyumba"

Mimi kama mack dizzo nilifanya " intro"

Akaimba Dada mmoja anaitwa " Queen darleen pamoja na dogo hamidu ambaye kwa sasa ndie anayejiita " yandu tozzy" pamoja na Dudu Baya lakini hatukuwahi kufanya nyimbo ya pamoja..

Maana kila mmoja alikuwa anakaa mtaani kwake na mara nyingi tulikuwa tunakutana kwenye matukio tu ..

Ingawa kuna nyakati mimi na Dudu Baya tulikuwa tunapenda kwenda pamoja studio kufanya project zetu kama solo Artist kila mmoja kivyake ..

🔥🔥🔥🔥🔥

ukwaju_wa_ kitambo
0767 542 202

#funguka.View attachment 3097040
TABIBU.

Ova
 
Back
Top Bottom