Albedo
JF-Expert Member
- Feb 24, 2008
- 5,558
- 1,456
Nimesoma kule kwa Michuzi kuwa zile tiketi za laki mbili zimeisha! Sijaelewa zilikuwa chache sana (kama 10 tu hivi) au ni watu wana mkwanja wa kufa mtu?
Janja ya TFF mkuu ili kuwafanya watu waone bei ya Kiingilio ni za kawaida mkuu, juzi nilikuwa nacheki habari kabla ya Mwakalebela hajatangaza Viingilio akanza kwa kusema kuwa tiketi za 200,000 zimeisha sasa nikajiuliza hao walionunua walinunua kwa Shilingi ngapi wakati hata bei zilikuwa bado kuwekwa hadharani nikapata hisia kwamba Hizo za VIP watakuwa wamepewa Bure Mawaziri na Viongozi wengine wa Kisiasa. Tufumbuke Macho Serikali inataka sisi Masikini ndio tubebe Mzigo wa Kuileta Brazil yaani ukimsikiliza Tenga unaweza kufikiri labla Tanzania Soccer Fans ndio wamewaandikia Barua TFF kuiomba Tanzania kuieta Brazil! Teh teh teh