Kiranga unamshambulia Charity wa watu kisa kaomba kuchangiwa aione mechi ya Brazil na Taifa Stars. Kwani kuna ubaya gani akiomba huo mchango na watu wakampa kwa hiari zao akaenda kuona?? Kwani kuna ubaya gani sana wa yeye angalau once in her lifetime aone Brazil ikicheza na nchi yake na kuishangilia nchi yake??? Kwani mtu haruhusiwi kufanya kile anachopenda ikiwa ni pamoja na kuangalia mpira LIVE kwa sababu tu Serikali imetumia taxpayers money(which ofcourse its not right) kuwaleta hao Wabrazil kucheza a friendly match??? What really is your point that you have been trying to make all this time???? (dont be a hater though usinishambulie na undiplomatic words/tone to say the least)
Kama unaona hakuna ubaya kuwa ombaomba then unanielimisha kwa nini nchi yetu ni masikini, wananchi wanaamini kuomba omba ni poa tu.
Halafu tunajidai tuna siasa ya kujitegemea.
Mimi binafsi napinga kuomba omba, sijamkataza kuomba hapa JF, ana haki ya kuomba, lakini mimi binafsi napinga.
Na kama yeye alivyo na haki ya kuomba, na mimi nina haki ya kukashifu na kukemea ombaomba wote.
Point ninayoimake ni kwamba nchi yetu itabaki masikini kwa miaka mingi, kwa sababu kuanzia serikali, chama mpaka wananchi hatujui fiscal responsibility.
Serikali inatumia $ 6 million kuileta Brazil kwa siku moja, serikali haina priorities. Tuna matatizo kibao yanayohitaji hizo hela na kuweza kuzitumia vizuri zaidi.
Wananchi wanataka kuishi maisha ya anasa kubwa kuliko mifuko yao inavyoruhusu, hawajui hata kufikiri, hawajui kwamba umasikini wao unatokana kwa sehemu kubwa na matumizi mabaya ya pesa za umma, hawaoni hata aibu kuja kuomba msaada ili kufanya anasa.
Point yangu ni kwamba kila siku tunaishambulia serikali ufisadi and all, kumbe hata wananchi wenyewe wanataka kuishi maisha ya kifisadi.Ukitaka kuishi maisha yaliyo juu ya uwezo wako unataka kuishi kifisadi, unaishi kwa tamaa.
Utaanza kuomba omba, utakuta watu wamechacha, utaanza kuiba au kuuza VISIVYOTAJIKA!!
Ndio ufisadi wenyewe huo.