Hard disk ya laptop naitumia kwenye TV shida inapata joto kali, natatua vipi hili tatizo ?

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
933
Reaction score
3,051
Hard disk ni ya laptop nimeiweka kwenye kasha limeandika Usb 3.0 ila waya wake ulikuwa mfupi, nikaunganisha huo waya na waya mwengine mrefu wa kuchomekea flash na external, waya nao umeandikwa usb 3.0.

Shida inakuja hard disk inapata joto kali sana
 
Kama waya ni mrefu iweke mahala ambapo itapata upepo ama itafutie kitu kiwe kinapulizia.
 
Nimeiweka sehemu yenye upepo na nipo mkoa wenye baridi Njombe.

Au labda waya au kasha vinachangia joto ? dukani niliona pia kuna nyaya ndefu na makasha yameandikwa "usb 2"
 
Nimeiweka sehemu yenye upepo

Au labda waya au kasha vinachangia joto ? dukani niliona pia kuna nyaya ndefu na makasha yameandikwa "usb 2"
Kuna nyaya za hivyo USB 3.0 Speed ni kama mita 1 tafuta zipo mbona kama upo Dar tafuta maduka ya electronics utazipata hata soko la Jiji naziona sana achana na za kuunga unga kienyeji, nafikiri hazizidi hata 15k niliwahi kua nayo 1 wahuni walinioteaga wakapita nayo kazini.

Hiyo uliyounga nafikiri kuna kitu utakua hujazingatia hasa kama nyanya zinatofautiana sifa ukubwa.. Hapo kuna Upotevu wa Voltage (Voltage Drop) Kuongeza urefu wa nyaya huongeza ukinzani wa umeme (Resistance), na kusababisha kushuka kwa voltage. Hii inaweza kufanya kifaa chako kifanye kazi kwa shida na kuleta ongezeko la joto.

Screenshot_20250508-232042_Jiji.co.tz.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Umeangalia size ya huo waja na uwezo wa wake wa kupitisha hiyo nguvu ya nishati ?
 
Nimeiweka sehemu yenye upepo na nipo mkoa wenye baridi Njombe.

Au labda waya au kasha vinachangia joto ? dukani niliona pia kuna nyaya ndefu na makasha yameandikwa "usb 2"
Kuna external case za type C zipo na cable unatumia hata USB ya kuchajia simu ile ya type C ni 3.0 speed pia, tafuta hizo kama vipi.
 
Kuna nyaya za hivyo USB 3.0 Speed ni kama mita 1 tafuta zipo mbona kama upo Dar tafuta maduka ya electronics utazipata hata soko la Jiji naziona sana achana na za kuunga unga kienyeji, nafikiri hazizidi hata 15k niliwahi kua nayo 1 wahuni walinioteaga wakapita nayo kazini.

Hiyo uliyounga nafikiri kuna kitu utakua hujazingatia hasa kama nyanya zinatofautiana sifa ukubwa.. Hapo kuna Upotevu wa Voltage (Voltage Drop) Kuongeza urefu wa nyaya huongeza ukinzani wa umeme (Resistance), na kusababisha kushuka kwa voltage. Hii inaweza kufanya kifaa chako kifanye kazi kwa shida na kuleta ongezeko la joto.

View attachment 3328411
Yaani ninatumia waya huo huo wa kwenye picha.

Halafu nimemuuliza chat gpt amesema usb 3 ina volty kubwa sana

Inaweza kuwa sababu ?
 
Yeah of course inapitisha umeme mwingi kiasi kuliko cable ya micro type B hizo 2.0.. na mara nyingi hizi TVs zetu unakuta by default zina ports za USB 2.0 so ka ukinzani (resistance) kapo kama ukiweka external ina 3.0 au 4.0 na lazima joto litokee.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Daah Chief bana nmecheka kwa hili eti aiweke mahala iwe inapata upepo....
HDD zina Overheat mkuu, kwenye pc kuna feni la Cpu na feni jengine maalum la vifaa vingine. Hdd iki operate zaidi ya 50C kuna hatari ya kupoteza hadi data ama kuharibika.
 
Ni kawaida kwa HD kupata joto hasa kwa matumizi ambayo ni continuous kama TV, maana yake ukiangalia movie inasoma kidodo kidogo muda wote hadi degree 50+C inaweza ikawa kawaida tu na haina madhara kama una wasiwasi sana unaweza kununua zile feni za PC au za USB ukaipachika juu ya HD, pia sidhani kama TV itakuwa ina USB 3, utakuwa unapata spidi ya USB 2 hata kama cable ni ya USB 3, kama video inacheza bila shida hakuna sababu ya kuhitaji 3 so tumia waya wowote ule.
 
Hapa umemaliza mleta mada apunguze mtero tu (Uoga) PC yangu hua naiweka External inapiga kazi siku nzima na haijawai leta shida yoyote, yeye asiende kuwa anaiskilizia joto limefika ngapi.
Pia Katika kifaa chochote cha Computer Backup ni muhimu aondoe vyovyote vya muhimu humo au awe na copy ya vile vya muhimu km vimo incase lolote likitokea.
 
Back
Top Bottom