Harmo Rapa atimua mbio baada ya Mh. Nape kuoneshwa bastola

Kama tumefikia kuwa kila kitu mtu anatoa bastola au SMG ndo mambo yaende tunaelekea kuzitumia sio kuzitoa muda utaongea
 
2020 atabaki na washambuliaji butu wasio na mbinu.
Ataishia kubadili katiba impe mamlaka kamili.
Nape kiukweli alipigania sana chama ........alikuwa ndio front man ....,sijui Kinana huko aliko atakuwa anajisikiaje kwakuwa ndio watu wawili waliobaki mstuni kupigania chama .....SAWA magufuli hamtaki maana hata uwaziri aliwapa kwa shingo upande ...lakini sio kumfukuza kwa namna hiyo
Kwani kulikuwa na ubaya gani kama kweli aliandika barua angemjibu tu kistaarabu na kumkubalia .....sasa hii inaweka wengine kama Januari na Mwigullu njia panda
 
Kutoka kukipigania chama kwa nguvu zote, mbunge, waziri mpaka kunyooshewa bastola kama gaidi hatari kisa kuitisha press conference. Wafia chama someni alama za nyakati, msitokwe tu na mipovu mitandaoni, hatima ya maisha yako ipo juu yako.
 
tumefikia hapa kutoleana bastola hadharani tena kwa kiongozi ? Hivi hawa watu wanaotumwa hayo mafunzo yanawasaidia nini ? Wanaokota wapi hizi takataka ,kulikuwa na sababu ya kutoa hiyo silaha na kukoki ?
 
Kilichonistua Inakuwaje Anaweka Risasi Kwenye Chemba, Halafu Anairudisha Kiunoni Na Kuanza Purukushani Ikifyatuka Je??.

Nani Aliyemfundisha Kuwa Matumizi ya Silaha za Moto Yako Hivyo?

Hili Jeshi Letu la Polisi Limejaa Wahuni Wengi Sana Kuanzia Ngazi za Juu Mpaka Hawa Askali Kanzu

Tanzania Inarudi Kwenye Dark Days Kama Mambo Yenyewe ni Hivi
 
Hivi alitoa bastola kwa ajili ya nini hasa? Lakini Nape upo imara Maana wengine wangekuwa wakimya kabisa lakini wewe umeongea!
 
Huyo kijana aliyetoa bastola anafahamika vizuri tu mbona hapa mjini? Tutamwambia Nape. Anafahamika hadi maeneo anayopendelea kwenda. Anajulikana sana hata kwa jina. Kuna mwana TISS mwenzake ni jirani yetu kwetu na ni rafiki wa huyu kijana. Ila hata wenzake huwa wanasema hajatulia kabisa. Huazimisha hata bastola kwa majambazi. Anafahamika vituko vyake.
 
Bastola yenyewe aliiweka mkono wa kushoto wakati yeye anatumia mkono wa kulia, huyu tiss hana uzoefu wa kutumia bastola, kwanza anaitoa bastola kishamba kabisa
Jinsi alivyotoa hiyo bastola inaonesha ni jinsi gani asivyo na maamuzi yenye akili, huwezi kuwa mtumizi wa mkono wa kushoto ukaweka bastola mkono huo huo.
Training gani hiyo? Unatoa bastola mpaka vest inaonekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…