Harmo Rapa atimua mbio baada ya Mh. Nape kuoneshwa bastola

Harmo Rapa atimua mbio baada ya Mh. Nape kuoneshwa bastola

huyo afisa hana uwezo...anatakiwa kufukuzwa. hajaona wenzie pale wametulia kimyaa? hivi anafikiri kwaakili yake angeweza kumuua nape pale mbele za watu? alifikiri nape ataogopa bastola wakati kuna watu wamejaa peupeee? hao ndio maafisa wetu tuliowafundisha? alitoa bastola kwaajili ya nini? kumtishia kwamba asipoenda ndani atampiga bastola? halafu taifa lingekuwa katika hali gani mbunge amepigwa bastole mbele za watu? huyo ni mjinga na anastahili kufukuzwa kazi. hajui kazi kwasababu kama angekuwa intelijensia mzuri kwanza wangemzuia hukohuko kabla hajafika hadi pale. wamesubiri hadi amefika pale ndio wanajifanya kuonyesha vimabavu vyao, kama wanamini kutumia nguvu ni ushidi waende iraq na syria huko wakakutane na wanaume wenzao.
 
Msanii Harmo rapa leo alienda kwenye kikao cha Mh. Nape kilichokuwa kinafanyia kwenye hoteli ya Protea. Baada ya kutokea sintofahamu askari/usalama alitoa bastola na kumnyooshea Nape Nnauye, tukio lile lilimpa wazimu Harmo Rappa na kujikuta anatimua mbio asijue aendako.
[HASHTAG]#HarmoBolt[/HASHTAG]
[HASHTAG]#BoltRappa[/HASHTAG]

solution sio kutimua mbio bali kutengeneza katiba mpya na tume huru ya uchaguzi itakayowafaa watanzania wote
 
Kama aliyeipigania ccm kiasi kile 2015 na alikuwa waziri wa serkali leo hii anatishiwa kupigwa risasi mbele ya halaiki!?hakika tunaelekea siko.
 
27777d2b983ac6e132ad3b3bef9ac6a0.jpg
Brilliant one....Kipanya alisharitabiri hili kabla, muda utatwambia.
 
Harmorapa alikuwa anakuja speed kumsalimia nape alipoona kuna sintofahamu akapunguza mwendo alipoona bastola .. Akaamsha popo ... Harmo wewe ni noma ila si wa kukutegemea kwenye ugomvi
 
Anapandishwa cheo kesho asubui wakati wa kuapishwa mwakyembe
 
.Mimi naomba wanausalama wachungane wenyewe kwa wenyewe,wasije wakauziana kesi.
Ukitumwa na mtu kwenda kwenye ishu nyeti kuwa makini kuelewa kama wote mliounda timu mna order ya aina moja toka mamlaka moja au...mtu unaweza kuponzwa hivi hivi.
That was simply a stupid move from a highly trained security officer,unaweza kuona jinsi wenzie walivyoreact negatively kwa alichokifanya huyo mwenye kofia
 
Day harmorapa kweli kaniacha hoi

Ila kitenge ni shujaa sana, mpaka jamaa akaufyata na kabastola make

Hao askari wapumbavu wa aina hiyo ndio wanafanya nchi hii we hapa
kumbe yule ni kitenge.....big up kwake
 
.Mimi naomba wanausalama wachungane wenyewe kwa wenyewe,wasije wakauziana kesi.
Ukitumwa na mtu kwenda kwenye ishu nyeti kuwa makini kuelewa kama wote mliounda timu mna order ya aina moja toka mamlaka moja au...mtu unaweza kuponzwa hivi hivi.
That was simply a stupid move from a highly trained security officer,unaweza kuona jinsi wenzie walivyoreact negatively kwa alichokifanya huyo mwenye kofia
Jamaa kachemka bigtime.
 
Si ili msimjue kirahisi, pia lazima utume mtambo vinginevyo mwenye akili timamu atakupotezea.
Aise Nape leo nimekukubali umekaa kidplomasia kabisa, nilikuwa sikujui vizuri. Hivi watu wanaona bastola ndio kitu cha kukimbilia?
 
Ha ha ha haa dah, kijana kaniacha hoi. Unajua kuna siku niliwahi kuwa mhanga wa scenario kama hiyo kwenye daladala, jamaa anajidai afisa usalama katoa bastola kumuelekezea kondakta wa gari nikashangaa watu wanashuka kwenye gari ghafla kupitia madirishani maana mlangoni ndio kulikuwa ugomvi huku mimi nimebaki nimezubaa sikujua kama bastola imetolewa...
Ila hawa jamaa huwa nawashangaa wanapogombana na watu kwanini hutoa bastola kutishia?

Malipo ya mambo yote ni duniani kwanza, ukisimamia haki Mungu atakuvika taji na mara mia duniani.
 
Unaona sasa jinsi Nape Nnauye alivyopuuza huo mkwara. Inaleta Ujumbe gani ukiachana na harmobolt usain

Hiyo move alishaijua mapema, na ukiangalia yule mwenye shati la pink waliekuja nae alikuwa seat ya nyuma na aliposhuka tu na kufunga mlango alimwacha Nape pale kama chambo vile, halafu yule kapero alipomfuata tu Nape na kutoa chuma, na yule aliyekuja na Nape alitaka kutoa chuma ila akaamua kusitisha na kumtuliza huyo mwingine, Mr Kapero. Halafu ukute Nape nae tayari alikuwa amevaa a bulletproof vest.

Hii movie ilivyokaa ni kama vile pale 'Victoria' na 'Mbweni' pamepasuka!!

 
Kweli leo Nape ni mtu wa kutishiwa na bastola tena mchana kweupe mtu ambaye alikuwa mjumbe wa baraza la mawaziri? hii ni zaidi ya hatari.
 
Back
Top Bottom