Harmonize alipwa milioni 23 kutumbuiza maonesho matatu nje ya nchi

10k ni show tatu za Canada ambazo ni nje ya Burundi kwahiyo jumla ni show nne ambazo malipo ya show tatu za canada ($10k) ni tofauti na hiyo ya Burundi japokuwa promota ni huyohuyo..nimekuwekea maelezo hapo chini
Nildhani ni mimi tu sijui kusoma. Hiyo $10K ni Burundi tu.

Hiyo pesa ni ya Show ya Burundi tuu.. according to maelezo

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app

Sijaelewa
Malalamiko ya promoter ni yepi haswa? Huyo Harmo kakiuka kipengele gani cha mkataba?

Naona tunajadili Konde Gang na WCB tu hapa
Wakuu hiyo habari ipo hivi


Promota wa shoo CHIMEZIE CHUKWUBUIKE ametoa malalamiko yake juu ya msanii wa Bongofleva Harmonize ambaye amekiuka makubaliano ya kufanya shoo.

“Nilimtumia Harmonize pesa kiasi cha Dola elfu kumi kwa makubaliano ya kufanya shoo kwenye miji mitatu Nchini Canada. Tulisaini mkataba nikaandaa kumbi katika miji mitatu lakini alianza kukwepa na akawa hataki tena kuzungumzia suala hilo”

“Kabla ya kuchukua pesa hiyo alikuwa akinipigia mara kwa mara nimpatie pesa akidai anataka kufunga ndoa na mpenzi wake na hakuwa na pesa.”

“Alikutana na rafiki yangu London akamtumia kuzungumza na mimi akitaka tubadili kutoka Canada badala yake tufanye shoo Nchi yoyote Afrika tofauti na Afrika Mashariki”

“Tulikubaliana kufanya shoo Guinea Bissau, nikahangaika na kupata eneo la kufanyia shoo lakini hakutokea.

“Nimefanya kazi na Diamond Platinumz mara kibao lakini sijawahi kuwa na matatizo naye, nimefanya kazi na wasanii wengi Wiz Kid, Kizz Daniel sijawahi kupata matatizo bao.”

“Nilijitolea kumsaidia Harmonize lakini hataki kufanya shoo na hataki kunilipa pesa zangu simu zangu hapokei wala jumbe zangu hajibu. Kwa sasa sitaki tena shoo naye, nimepoteza kuandaa venue lakini sio tatizo nataka anilipe pesa zangu.”

“Polisi Nchini Tanzania wanafahamu kisa hiki kupitia kwa wakili niliyemwita kushughulikia kesi hii anaitwa Sabastian.” ameongea Chukwubuike kwa uchungu mkubwa.

#KitengeUpdates
 
Kimsingi Harmo kakosea sana
 
Malipo ya $10k ni kwa show ya Burundi pekee...na hiyo show ilipangwa mwezi wa 8...

Sasa iweje shutuma zitajwe miezi miwili baadaye?

Otherwise hizi ni porojo
 
TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO
HARMONIZE ATOKOMEA NA MILIONI 23++ ANADAI AMEFULIA VIBAYA ANATAKA YA KUFUNGIA HARUSI.

PROMOTA WA SHOO KATANGAZA HALI YA HATARI KWA HARMONIZE KWAMBA ATAJAZWA MTU MIMBA ZA UTOTONI.

YASEMEKANA MAGUNIA YA BANGI YAMEONGEZEKA NYUMBANI KWA HARMONIZE BAADA YA KUTOKOMEA NA HIZO MILIONI 23.
 
Kama huu ndio mkataba wewe ndio unakosea kuna neno "ONLY FOR" katika hichi kipengele. Linabainisha hiyo 10k ni ya Burundi pekee. Labda kama sio kiingereza ninachokijua mimi au wenzangu walio jaribu kukuelewesha hapo juu.
 
Sasa si Bora angebaki wasafi achukue asilimia 40 ...wasafi angekuwa analipwa zaidi ya dollars elfu 50 Kwa show hata akichukua asilimia 40 it's better

Na anaenda na group kubwa wakiongozwa na kajala
 
Kama huu ndio mkataba wewe ndio unakosea kuna neno "ONLY FOR" katika hichi kipengele. Linabainisha hiyo 10k ni ya Burundi pekee. Labda kama sio kiingereza ninachokijua mimi au wenzangu walio jaribu kukuelewesha hapo juu. View attachment 2395302
Mkuu usibishane na mimi bhn hayo maelezo niliyotoa mimi nimeyacopy kwenye page ya kitenge yeye ndiye aliyefanya mahojiano na huyo promota na hayo ndio prodyuza aliyasema..mengine kuhusu mkataba sifahamu aisee labda tumsikie na harmo nae
 
Mkuu usibishane na mimi bhn hayo maelezo niliyotoa mimi nimeyacopy kwenye page ya kitenge yeye ndiye aliyefanya mahojiano na huyo promota na hayo ndio prodyuza aliyasema..mengine kuhusu mkataba sifahamu aisee labda tumsikie na harmo nae
Sijabishana nawe kaka, tunaeleweshana tu. Kitenge na huyo promota wote binadamu kama sisi. Mimi nakuomba rejea hayo makubaliano ya kimaandishi (mkataba) utaelewa hoka yetu ulipo.
Kitenge amesharipoti habari nyingi tu ambazo hazina ukweli.
 
Mtumizi ya msanii usilinganishe na mimi nnae tumia 10000/- kwa sku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…