Katika hali isiyokuwa ya kawaida aliyekuwa msanii namba mbili WCB na nchini Tanzania kwa ujumla bwana Harmonize ameendelea kutudhihirishia kuwa kuna nguvu ya ushawishi mitandaoni imepungua katika muziki wake baada ya kujitoa kwenye lebo hiyo kubwa Tanzania!
Mara baada ya kuachia Album yake ya kwanza nnje ya WCB na kuachia video ya kwanza MAMA kwenye album hiyo tumeona kwa mara ya kwanza Harmonize akisuasua na kushindwa kufikisha viewers 1M hata baada ya wiki kupita!
Wakati hayo yakiendelea wasanii Rayvanny na Mbosso ambao bado wapo chini ya lebo hiyo kubwa nchini wao wameendelea kumtambia msanii Harmonize kwa kumkibiza mbali sana kwa viewers wengi sana kwa muda mfupi tangu watoe nyimbo zao!
Harmonize juzi aliandika huko instagram kuwa kutokana na kuwa tayari album yake ina video za nyimbo zote atalazimika kuachia video mara baada ya mojawapo kufikisha 1m viewers!
Sasa kutokana na ugumu anaoupata kufika viewers hao ameamua tu kuachia video ya Bedroom hata kabla video ya Mama kufika 1m.
Kwa pamoja tumuunge mkono atoboe sawasawa na yaliyokuwa malengo yake wakati anajitoa USAFINI!!!!
View attachment 1402239View attachment 1402240
Sent using
Jamii Forums mobile app