Kwa nini kuondoka Harmonize mnachukulia kama vita.Mimi mwenyewe nafurahi Harmo kujitegemea mwenyewe ,tatizo je amejipanga kwa fitina ?Usimwone Mondi ana shine jua nyuma ana watu wanampigania je yy anao?Kama anao ni kitu kizuri kama hana yy ndiye atakaye umia.Msimwone Belle 9 yupo kimya mkazani hana uwezo bali hana watu wakuupigania mziki wake.
Kuwa chini ya label ni kitu kizuri sana ,haswa kwa wenzetu US,Drake yule pamoja na kuwa na utajiri mkubwa,label yake ya OVO lakini bado yupo chini ya YCMB,we unazani kwa nini Drake hajaondoka YCMB label ya Lil Wyne na Birdman?
Kanye west ana label ya Good Life,ana brand ya Yeezy ambayo thamani yake ni zaidi ya USD 1 bilion,lakini pamoja na utajiri wake bado yupo chini ya Roc Nation ya Jay Z,hujajiuliza kwa nini Kanye bado yupo chini ya Roc nation?
Rihanna sasa hivi networth yake USD 600m baada kama ya miaka mitatu au miwili atakuwa na USD 1bil ,lakini bado yupo chini ya Roc Nation ya Jay Z,wewe unazani kwanini Rihanna,Drake,Kanye West na hata Nick Minaj pamoja na utajiri wao lkn bado wapo chini ya label?
Label zina umuhimu wake sana sababu katika Industry hizi za Music kuna FITINA na KUBANIANA ,kwani kuna watu wakali lkn hawana watu wa kupush mziki wao.
Miaka ya nyuma kulikuwa na mwanamziki wa RnB Bob Valentino alivuma sana alipokuwa chini ya DTP Ludacris,baadaye akaondoka akamwambia Luda anataka kujitegemea,baada ya hapo Bob V akapotea mazima.
Vile vile kulikuwa na Rapper Chingy nae alikuwa DTP akazinguana na Luda,akwambia yeye anaondoka anataka kujitegemea Ludacris kamruhusu nae akapotea mazima
MTV brings viewers the best in lifestyle and competition reality shows, plus live events featuring the biggest names in entertainment.
www.mtv.com
na nasikia hata Runtown wa Nigeria kapotea baada ya kuondoka kwenye Label.
Kuanzisha label au kujitegemea sio swala baya kwani hata yy anaweza wafungulia mlango wengine,lkn je amejipanga,mziki huu mgumu kwani umejaa fitina ,unahitaji watuwanaojua industry ili upush kazi zako.
Na ndio maana pamoja na kuwa na mihela yao wakina Rihanna,Kanye,Drake na Nick Minaj bado wapo chini ya Label.
Na Mziki wa Tz sasa hivi una hali mbaya yaani washikadau wamewagawa mashabiki,siku hizi team za kwenye mziki wetu,hazina utofauti na ushabiki wa Simba na Yanga,ili upate support unatakiwa uwe ndani ya hizi team,ukiwa nje umekwisha mfano tu Baraka da prince na Mavoko tushaanza kuwasahau.