Man unaelekea hutaki kukoselewa manake kila aliyekukosoa, mara umuite Bi Sandra, mara umuite Tanasha!!!
Kuna mtu kakwambia hizo habari za Diamond siku zake zimeisha, na mwenyewe umemuita majina ya kuchukiza! Man, penye kukosolewa kubali kukoselewa! Hebu soma hii habari: Hiyo ni habari ya mwaka 2013, nami kamkumbuka huyo Yahya alisema hayo wakati akihojiwa na EATV. Miaka 6 imepita lakini Diamond aliyesema alikuwa hapewi hata shows za 7 Million, leo hii hata kwa 20 million hapigi show! Na threads za kutabiri kuanguka kwa Diamond zipo hapa JF kwa miaka kadhaa sasa, lakini jamaa yupo pale pale!!!
Hata hivyo, nakubaliana na wewe kwamba Harmonize bila WCB sio Harmonize! Na akitaka asahaulike ndani ya mwaka 1, atoke WCB!
Binafsi, simkubali kabisa Harmonize! Namwelewa zaidi Rayvann ambae yupo unique kuliko Harmonize ambae ni clone ya Diamond! Almost anaiga kila kitu kutoka kwa Diamond!