Hii thread ni baada ya minong’ono ya Harmonize kuondoka WCB kuzidi kupamba moto , narudia tena ni baada ya Minong’ono maana mpaka sahizi hakuna official statement kutoka pande yeyote ile .
Sasa basi, kama ikija ikatokea Bwana Harmonize akaondoka WCB wakati huu ana option moja tuu mezani kwake na yenyewe ni kuwa mchafu sababu amekataa kuwa Msafi.
Hii ni kutokana na muziki wa Bongo fleva kugawanyika katika Blocks mbili kubwa .... , BLOCK ya kwanza ni ya wasafi ambao ndio wanaonekana kuukamata muziki wa Bongo kutokana na ngoma zao kutamba zaidi nje na ndani ya Tz licha ya kutopata promotion kwenye media nyingine kubwa hapa Tz.
BLOCK nyingine ni hiyo ya WACHAFU(kinyume cha Wasafi) wao wanaongozwa na kampuni ambayo imekuwa ikiyaendesha masuala ya Burudani hapa Tz kwa muda mrefu sana, kwa sasa hii BLOCK imebakiwa na uzoefu tuu sana sana kwa kuwa haina Galacticos (mastaa) wa kutosha kama ile BLOCK ya wasafi.
BLOCK ya wasafi imeweza kupambana na kutawala muziki licha ya ugumu wa kunyimwa promotion na media houses kubwa karibia zote kutokana backup kubwa ya mashabiki wanaowasupport na kuwepo na viongozi ambao wanazijua fitna za muziki wa hapa nchini bila kusahau Diamond Platnumz ambaye ni msanii nambari 1 nchini ameweza kuwasambaza mashabiki wa kazi zake wakasupport kazi za vijana walio chini ya label yake Kwahiyo ikawa rahisi sana kwa wanamuziki kutoka hii Block kutamba Hata kama ngoma zao hazichezwi kwenye media houses kubwa.
#TujekwaHarmonize
Huyu bwana alipigwa fitna sana kabla hizi Blocks hazijawa kubwa kiasi hichi lakini aliaminika watu wakamwaga hela kuwekeza kwenye kipaji chake akaslide na upepo wa label pamoja na juhudi zake akawa msanii namba 2 pale katika Block yao, lakini kadri siku zinavyoenda minong’ono ya yeye kutaka kujitegemea inazidi mkubwa mikubwa.
Swali la kwanza la kujiuliza , Je Harmonize amefikia ukubwa wa kuweza kujitegemea mwenyewe na kusurvive nje ya hizi BLOCKS 2 ?...................... kwangu jibu ni Hapana , hajafikia huo ukubwa isitoshe akihama ataacha mashabiki wengi sana pale pale kwenye BLOCk yake .
Swali la pili la kujiuliza, Je Harmonize atakuwa na backup ya kina nani wanaojua fitna za huu muziki wetu?
Kwangu jibu ni sijui, maana wataalam wa hizi fitna wapo BLOCKS hizi mbili hasa hasa BLOCK ya wasafi.
Swali la tatu la kujiuliza, Je BLOCK ya wachafu watamuunga mkono Bw Harmonize wakiamini kutaidhoofisha BLOCK ya Wasafi?
Kwangu jibu ni sijui, lakini kwa akili ya kawaida adui/mpinzani wa adui yako ni rafiki yako, so anything can happen.
Kwa muktadha huu kama Harmonize anaitaka #1 aliyopo Diamond option aliyonayo ni kuwepo BLOCK ya wachafu, lakini kama atakuwa comfortable na #2 atulie zake hapo WCB huenda upepo ukabadilika siku moja lakini kuhamia BLOCK ya wachafu kuna risk zake maana kule atapata support ya kinafki tuu siku wakimchoka anatupwa kule na isitoshe hakuna guarantee ya kumtoa Diamond #1 kwa sababu BLOCK ya Wachafu wamehangaika miaka kadha wa kadha kumng’ofoa Diamond #1 ila imeshindikana.
N.B , Haya ni maoni yangu tuu wala sina nia ya kumtisha Bw. Harmonize kama ataamua kuhama sawa tuu ahame, maana mwisho wa siku atapambana na hali yake sisi mashabiki tunataka muziki mzuri na akizingua anawekwa kapuni tuu kama kina Mavoko..