Harmonize it’s either uwe MSAFI au MCHAFU

Harmonize it’s either uwe MSAFI au MCHAFU

Wabongo vilaza kweli kweli .. Drake ametoka na hapakuwa drama tuache harmo kutoka wcb ..nyiye mnataka jama aendeleye kuburuzwa sa salam na babutale ...mtoto akikuwa lazma ahame kwake
Acha uongo Drake pamoja na kuwa na label yake ya OVO bado yupo chini ya YCMB na Kanye west pamoja na kuwa na label yake ya Good life na brand yake yeezy yenye thamani ya zaidi ya USD 1bilion bado yupo chini ya Roc Nation ya Jay Z.
 
Wabongo vilaza kweli kweli .. Drake ametoka na hapakuwa drama tuache harmo kutoka wcb ..nyiye mnataka jama aendeleye kuburuzwa sa salam na babutale ...mtoto akikuwa lazma ahame kwake
Drake hadi leo yupo chini ya young money cash monry label.
 
Kwani hiyo block ya wasafi si kuna baadhi ya wasanii wapowapo tu wala hawana lolote? Mfano yule queen si dam moja kabisa na mond? Na umesema hiyo block ina wazee wa fitna kuliko block ya uchafuni kwa sasa? mbona hatuoni akimfunika hata amber ruti ? Me nadhani pamoja na fitna za hapa na pale, kipaji nacho kina nafasi yake kwa kiasi kikubwa tu. Japo akijitoa mambo yanaeza yasimwendee poa kama matarajio ya wengi yalivyo. Ajaribu tu then tutajua mbele kwa mbele tunachotaka sisi mashabiki ni mziki mzuri basi.
 
Hii thread ni baada ya minong’ono ya Harmonize kuondoka WCB kuzidi kupamba moto , narudia tena ni baada ya Minong’ono maana mpaka sahizi hakuna official statement kutoka pande yeyote ile .

Sasa basi, kama ikija ikatokea Bwana Harmonize akaondoka WCB wakati huu ana option moja tuu mezani kwake na yenyewe ni kuwa mchafu sababu amekataa kuwa Msafi.

Hii ni kutokana na muziki wa Bongo fleva kugawanyika katika Blocks mbili kubwa .... , BLOCK ya kwanza ni ya wasafi ambao ndio wanaonekana kuukamata muziki wa Bongo kutokana na ngoma zao kutamba zaidi nje na ndani ya Tz licha ya kutopata promotion kwenye media nyingine kubwa hapa Tz.

BLOCK nyingine ni hiyo ya WACHAFU(kinyume cha Wasafi) wao wanaongozwa na kampuni ambayo imekuwa ikiyaendesha masuala ya Burudani hapa Tz kwa muda mrefu sana, kwa sasa hii BLOCK imebakiwa na uzoefu tuu sana sana kwa kuwa haina Galacticos (mastaa) wa kutosha kama ile BLOCK ya wasafi.

BLOCK ya wasafi imeweza kupambana na kutawala muziki licha ya ugumu wa kunyimwa promotion na media houses kubwa karibia zote kutokana backup kubwa ya mashabiki wanaowasupport na kuwepo na viongozi ambao wanazijua fitna za muziki wa hapa nchini bila kusahau Diamond Platnumz ambaye ni msanii nambari 1 nchini ameweza kuwasambaza mashabiki wa kazi zake wakasupport kazi za vijana walio chini ya label yake Kwahiyo ikawa rahisi sana kwa wanamuziki kutoka hii Block kutamba Hata kama ngoma zao hazichezwi kwenye media houses kubwa.

#TujekwaHarmonize

Huyu bwana alipigwa fitna sana kabla hizi Blocks hazijawa kubwa kiasi hichi lakini aliaminika watu wakamwaga hela kuwekeza kwenye kipaji chake akaslide na upepo wa label pamoja na juhudi zake akawa msanii namba 2 pale katika Block yao, lakini kadri siku zinavyoenda minong’ono ya yeye kutaka kujitegemea inazidi mkubwa mikubwa.

Swali la kwanza la kujiuliza , Je Harmonize amefikia ukubwa wa kuweza kujitegemea mwenyewe na kusurvive nje ya hizi BLOCKS 2 ?...................... kwangu jibu ni Hapana , hajafikia huo ukubwa isitoshe akihama ataacha mashabiki wengi sana pale pale kwenye BLOCk yake .

Swali la pili la kujiuliza, Je Harmonize atakuwa na backup ya kina nani wanaojua fitna za huu muziki wetu?

Kwangu jibu ni sijui, maana wataalam wa hizi fitna wapo BLOCKS hizi mbili hasa hasa BLOCK ya wasafi.

Swali la tatu la kujiuliza, Je BLOCK ya wachafu watamuunga mkono Bw Harmonize wakiamini kutaidhoofisha BLOCK ya Wasafi?

Kwangu jibu ni sijui, lakini kwa akili ya kawaida adui/mpinzani wa adui yako ni rafiki yako, so anything can happen.

Kwa muktadha huu kama Harmonize anaitaka #1 aliyopo Diamond option aliyonayo ni kuwepo BLOCK ya wachafu, lakini kama atakuwa comfortable na #2 atulie zake hapo WCB huenda upepo ukabadilika siku moja lakini kuhamia BLOCK ya wachafu kuna risk zake maana kule atapata support ya kinafki tuu siku wakimchoka anatupwa kule na isitoshe hakuna guarantee ya kumtoa Diamond #1 kwa sababu BLOCK ya Wachafu wamehangaika miaka kadha wa kadha kumng’ofoa Diamond #1 ila imeshindikana.

N.B , Haya ni maoni yangu tuu wala sina nia ya kumtisha Bw. Harmonize kama ataamua kuhama sawa tuu ahame, maana mwisho wa siku atapambana na hali yake sisi mashabiki tunataka muziki mzuri na akizingua anawekwa kapuni tuu kama kina Mavoko..
ALIKUWA HAPO HATA KABLA YA KUMFAHAMU, ANAZIJUA HUSTLE ZAKE,ANAZIJUA NJIA ZAKE, TUACHE KUWEKA UKOMO WA MAFANIKIO KUWA UKITOKA SEHEMU FULANI HUWEZI KUTOBOA TENA, TUSIKARIRI NJIA ZA MAFANIKIO KTK MAISHA YETU, NOTION YA KUSEMA BILA WATU FULANI SIFIKI PALE, HII NI NOTION YA KIPUMBAVU, UBAYA MZIKI WA BONGO UNAFIKI NI MWINGI KUANZIA MASHABIKI WENYEWE, WENYE DHAMANA YA HUU MZIKI, NA UZWAZWA WA MSANII MWENYEWE, UKIJITOA SEHEMU FULANI KUNA KUNDI LA WATU WANATAKA KUKUSHUSHA, UKIWA SEHEMU FULANI NAPO KUNA KUNDI LA WATU WANAKUAMINISHA KUWA HAPO NDIPO MAHALA SAHIHI HADI PALE MASIHI ATAKAPOSHUKA, HAYA NI MAWAZO UHARO YALIYO KATIKA TASNIA YETU, UTHUBUTU NI MDOGO, UOGA, KUANGALIA WENGINE WATAKUSEMAJE UKIWA VILE, KUAMINISHWA MAISHA YAKO YA MZIKI HAYAWEZI KUFIKA KOKOTE BILA KAMBI FULANI, NDIPO UNAKUJA KUAMINI MSEMO HUU KUWA "YOU CAN'T BE FREE IN AFRICA UNTIL YOU BECOME A PUPPET OR HYPOCRITE". kwa mtindo huu umataifa tutasikiaga kwenye bomba tu, wakati bongo furaha iko kupeleka wasanii 3 kama si wanne ktk tuzo za kimataifa wenzetu Nigeria wako kama ,30 kama si 50 kimataifa😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Alafu tunajisifiaaaaaaa😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Wabongo vilaza kweli kweli .. Drake ametoka na hapakuwa drama tuache harmo kutoka wcb ..nyiye mnataka jama aendeleye kuburuzwa sa salam na babutale ...mtoto akikuwa lazma ahame kwake

Kwanza nianze kwa kushukuru kwa kutuita wabongo vilaza maana umejumlisha na wazazi waliokuzaa.

Kingine ukiwa unalinganisha vitu Jaribu kufanya mlinganyo kwa vitu vinavyofanana ama sivyo utaonekana kilaza zaidi ya unaowaita vilaza.

Kwa mfano, hapa unataka kulinganisha muziki wa Bongo na wa Us ???

Una akili timamu kweli !!.

Muziki wa bongo bado sana kufika huko, hapa kwetu industry ipo chini ya vichwa kadhaa tofauti na hapo imekula kwako .
 
Kitu ambacho Nafikiri ni kwamba Harmonize amekuaa kimuziki na kimapato lkn WCB wamegoma ku update Mkataba wake ndomana anaona kama anafanya kazi kubwa halafu matokeo madogo... (Nafikiri hivyo)
 
Mavoko mikataba ya kijinga ndo imemuua
 
Mikataba waliyoingia nayo inawabana ndo maana wanajitoa

Kitu ambacho Nafikiri ni kwamba Harmonize amekuaa kimuziki na kimapato lkn WCB wamegoma ku update Mkataba wake ndomana anaona kama anafanya kazi kubwa halafu matokeo madogo... (Nafikiri hivyo)
 
Kwani hiyo block ya wasafi si kuna baadhi ya wasanii wapowapo tu wala hawana lolote? Mfano yule queen si dam moja kabisa na mond? Na umesema hiyo block ina wazee wa fitna kuliko block ya uchafuni kwa sasa? mbona hatuoni akimfunika hata amber ruti ? Me nadhani pamoja na fitna za hapa na pale, kipaji nacho kina nafasi yake kwa kiasi kikubwa tu. Japo akijitoa mambo yanaeza yasimwendee poa kama matarajio ya wengi yalivyo. Ajaribu tu then tutajua mbele kwa mbele tunachotaka sisi mashabiki ni mziki mzuri basi.

Mkuu unachosema hapa kimeandikwa kwenye paragraph ya mwisho
 
Mashabiki wapo hata wa wasafi.. kwani umeona kila shabiki wa wao wanawashadadia wote?
Nchi ina wananchi wengi ni mtu na juhudi zake kujiongeza kwa njia zinazofanyika ktk kazi yake..

Hehe unachukulia poa fitna za muziki wa Bongo
 
Ndio anachotaka kufanya harmonize icho
Acha uongo Drake pamoja na kuwa na label yake ya OVO bado yupo chini ya YCMB na Kanye west pamoja na kuwa na label yake ya Good life na brand yake yeezy yenye thamani ya zaidi ya USD 1bilion bado yupo chini ya Roc Nation ya Jay Z.
 
Hivi nyie kwa akili zenu mnaamini kabisa harmonize anaweza kuondoka WCB?!??
 
Back
Top Bottom