Harmonize kamrudisha Rich Mavoko kwenye game upya

Ila Neyo alipotea kama akina R Kelly
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanashindwa kubadilika na kufuata kizazi cha sasa kinataka nini. Na wengi hawabadiliki sababu ya kiburi cha kuamini wao hawawezi kuwafata watoto wadogo namna wanavyoimba kwa sasa wakati wao ndio wameuweka mziki Wa bongo flavor kwenye ramani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 



Ndio maana wanaita music industry. Kama una kipaji cha kuimba, peke yako huwezi kufanya kile kinachotegemewa na wengi, lazima ukubali kugawana mkate na wengine kwenye ufanisi. Kwani hata hao wenye majina makubwa kwenye tasnia hii wana team wanayofanyakazi pamoja.
Wakubali kuandikiwa nyimbo, kuwe na vocal coaches wa kuwasaidia, wakubali kukosolewa, wawe wavumilivu. Kwenye uvumilivu naongea kuhusu patience. Wasikimbilie kurekodi baada ya wiki moja ngoma iko youtube, inabidi wahakikishe ubora kwanza kabla ya kutoa muziki. Kuna mambo mengi. Ushirikiano kwenye kazi yoyote ni muhimu, waache chuki binafsi kati yao, hii haisaidii. Kuna vitu vingi vinawarudisha nyuma lakini hawajui.
 
Hakuna msanii bongo aliyewahi kupotea na akarudi kwenye game.. labda mavoco ndio awe wa kwanza...
Ukipotea inabidi ufanye ustaalabu mwingine utoke kivingine kama ni bussiness n.k.

Sasa hivi kwenye game kuna damu changa. Sasa kutushawishi tuendelee kukusikiliza ni kazi sana..
Walijaribu wakina Abby skills , Q chief , GK ,beka , hussein machozi n.k lakini game bado halieleweki..

Labda yeye ataweza.
 
Fact
 
ko keshapata management ya kupush kazi zake..?
 
Ali Kiba aliwahi kupotea kisha akarudi kwa kasi na kisha kaishia kuimba ujinga ujinga tu sahzi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ko keshapata management ya kupush kazi zake..?
 
Mmakonde kufata upepo.kabla ya kumaliza ichi ana kimbilie ichi.mwisho wa siku mambo yake yana kua haya eleweki
 
Hivi Wasanii ambao walikuwa wanategemea muziki tu,ambao hawana biashara nje ya muziki kipindi hiki wanaishije? Au Caller Tunes,Youtube Views etc?
 

Ukisema hakuna Dully Sykes unamuweka wapi mkuu au FA Pia !!!....
Kuna watu wapo flexible na hawachuji..

Kwanza damu changa za maana zinahesabika, wengi wanaimba kwa kucopy kiasi ukiweka playlist unaweza usitofautishe sauti, melodies na mashairi yao.
Hapa ndo WCB wanaendelea kuwin na kutawala music industry zaidi maana kila mtu anacheza tune yao
 
FA ,Dully,Blue hawajawahi kupotea kwenye game..
 
Kila nikisikia kokoro,Namvulia kofia Richadi.
Kipaji halisi!
Hivi harmonize kweli yuko humble kama anavyojionesha au ni public sympathy anatafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…