Harmonize kamrudisha Rich Mavoko kwenye game upya

Harmonize kamrudisha Rich Mavoko kwenye game upya

Tatizo la Harmonize ni moja tu kudandia dandia mambo(jumping jumping no Position),hana consistence ndio mana kila anapotia mkono panafeli,kwa nini asifocus kwenye jambo moja alimalize then ahamishie nguvu kwa jambo jingine...Ibra mwenyewe kashindwa kumpromote.
 
Kwani kupotea unavyoelewa ina maana gani.. kuishiwa au kukaa muda mrefu bila kutoa wimbo wowote
Kuishiwa yaani hata ukitoa ngoma haifiki popote.. mfano mavoko sasa hivi sio kwamba hatoi ngoma. Juzi kati hapo alitoa ngoma lakini haikufika popote.

Cheki mtu kama baraka da prince alitoa ngoma week 2 ilikua na view kama 2k .. huyo ndio kapotea..

Lakini kuna wasanii wao sio watu wa kutoa ngoma juu ya ngoma kama FA , AY n.k lakini sio kwamba wamepotea na siku wakitoa zinafanya vizuri tu

Screenshot_20200506-125727.jpg
 
Kila nikisikia kokoro,Namvulia kofia Richadi.
Kipaji halisi!
Hivi harmonize kweli yuko humble kama anavyojionesha au ni public sympathy anatafuta.
Public sympathy Kama kawaida yake.
 
Ningemshauri huyu Konde kupunguza papara...
Hakuna kitu chochote kafanya na huyo Ibrah. Kwenda kwa Mavoko ni kutafuta cheap popularity na public sympathy.. Hakuna mahali atafika.

Hawezi kumprove Bin Laden wrong... He has to fight to prove himself right.
 
Hivi ni kwanini kila Harmonize akiandika anapenda kuonyesha kulalamika ndani ya maandishi yake? Kwanini anajionyesha kama mtu wa malalamiko sana?
Anatafuta huruma ya jamii.. Akili kama za Kiba.
Hakuna mahali atafika.
 
Hivi ni kwanini kila Harmonize akiandika anapenda kuonyesha kulalamika ndani ya maandishi yake? Kwanini anajionyesha kama mtu wa malalamiko sana?
Kama anavyofanya alikiba tatizo la public sympathy haidumu na watu wakijua Hilo wanakupotezea.
 
Mwaka jana alisema anamrudisha Q chillah vipi wameishia wapi?
Mambo vipi!

Kama unavojua rich mavoko aliondoka wasafi na kuanza kujitegemea, lakini hajawahi kutoa ngoma wala kuskika kama mwanamuziki mkubwa! sasa harmonize amesema kuhusu mchizi!

Familia ngapi zipo nyuma ya Rich Mavoko na zinamtegemea yeye kwakila jambo hasa hili la kupata mkate wa kila siku vp kuhusu ndoto za familia hizo na zinaishije katika wakati huu?

Ndoto ngapi za wasani ambao wanategemea kuzifikia hizo ndoto kupitia mavoco na nyuma ya hao wasanii kuna familia nyenginepia

Je, maumivu malala miko ya wazazi wake hasa mama mzazi ambae ndio kama roho yake ushajiuliza ni kauli ngapi za uchungu anazitoa ambazo zinaweza kumpata kila anaefurahishwa na hili kwa makusudi

Mana mzazi wa mwenzio ni wako pia laana yake haishindwi kukupata. La mwisho kabisa mgeukie mwenzio anaefurahia na kuifanya hii kuwa ni habari njema kwake ya kumfanya atembee kifua mbele na hata kuandika mtandaoni kwa furaha Mavoko kapotea muulize anafaidika na nini?

Mungu anasababu na maana yake bro Rich Mavoko kama mdogoako nakuombea najua ukimya wako unamaana kubwa sanaa ndani yako ninachojua ni kujiweka sawa na kutuletea kazi zingine tunakupenda na tunakuombea mungu akufanyie wepesi. Let's go bro mdogoako rafiki yako nipo hapa muda wowote.

Ramadan Kareem

View attachment 1441196

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi qchief ndo qchilla?
Hayo maneno ameyaandika Huyu huyu harmonize,ambae alitaka kumrudisha Q chief kwenye game mwishowe akashindwa vibaya sana na kumtelekeza Q chief wa watu na Tangu konde kafungua Kondegang hataki hata kumpost Q chief

Haya mambo ya kumsimamia msanii ni magumu sana,harmonize alishaprove failure kwa Q chief sioni akileta jipya kwa mavoco.
ni kupuuzia tu, maana hata ibraa tz,ameshindwa kumweka level ya hata ya Zuchu kwenye trending huko streaming platforms,maybe Ngoja tuone hiyo ijumaa.

Najua ni nje ya mada lakini umeicheki avatar yangu mkuu?
 
Nikiangalia hiyo post naona kabisa Harmonize anatafuta attention ya watu na si msaada halisi kwanza ameandika kanakwamba huyo jamaa anaoneswa na anafanyiwa figisu....na hata ukiuliza ni akina nani wanaofanya figisu lazima watahusishwa WCB ila la kujiuliza mbona Richard Mavocko alipotoka alikua ana sapoti kubwa ya redio zote kubwa iweje sasa kikundi cha watu wachache ndo kionekane kinambania...

Nitakua wa mwisho kuamini huu msaaada kama una lengo sahihi zaidi ya kutafuta attention ya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipi huwa kinasababisha wasanii wa nyumbani wakianguka na wasiinuke tena? Tungo zao ni zilezile hawawezi kubadilisha ladha ya muziki wao au.

Ferouz alijaribu kuinuka akabaki chini pale. Q Chilla hadi leo yupo chini licha ya uwezo mkubwa wa kuimba alionao. TID naye hivyohivyo japo ukubwa wa J Nature umemsaidia hata akipata collabo anafanya kitu chenye kuonekana.

Tatizo ni nini kwa wasanii wetu ni kwamba hawana namna ya kurudi wakishuka kimuziki au mashabiki huwachoka mapema na kuwashusha wao wenyewe? Sioni Rich Mavoko akitafuna mfupa uliowashinda wengi.
Kingine ni kutojua nani wateja wa miziki yao, umri unavyokuwa vile vile na mashabiki zako, lkn pia muziki wako unatakiwa uendane na umri wa shabiki zako. Ndio maana akina msondo na sikinde wamepoa sio sababu hawajui muziki ila wale mashabiki zao sasa hivi ni watu wazima hivyo ilibidi wajitune kutokana na hilo. Hata Diamond nk nk umri ukienda itafika mahali madogo hawatawakubali na wakubwa pia hawatawakubali, sabaabu watatokea madogo wengine wakali kuliko wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haiwezi kufanya muziki wake urudi yaani Tanzania ukiteleza katika muziki itatumika nguvu kubwa sana kukurudisha.

Baada ya Darassa kutoa wimbo Safari na Muziki alijikakamua kutoa nyimbo zaidi ya 3 ila hazikuwa kama zile na watu wakaona Darassa alijishusha mwenyewe kwa kushindwa kuleta upinzani kwenye wimbo wake mwenyewe. Sasa Rich Mavoko haitaji collabo na Diamond au Harmonize ili arudi katika game ya muziki ila anatakiwa ajue zamani aliweza vipi na afanye nini amerudi kuwa pale alipodondokea.

Rich alifanya kazi na Diamond ila kwa muda mchache wimbo una-hit na kufutika katika anga la burudani leo hata afanye kazi na wasanii mwenye ushawishi anaweza akatumika kumwongezea ushawishi huyo atakaeimba naye.

Kikubwa asimame mwenyewe aone kama ataweza ila akianza kusimama kwa kutaka collabo na wengine je atarudia nao collabo ngapi ili azidi kuwa juu kimuziki.
Hii bonge moja la point aisee. Natamani mavoko a.k.a mesi wa bongofleva asome huu ujumbe wako. All in all tunamuombea arudi tena kwenye game.
 
Kuishiwa yaani hata ukitoa ngoma haifiki popote.. mfano mavoko sasa hivi sio kwamba hatoi ngoma. Juzi kati hapo alitoa ngoma lakini haikufika popote.

Cheki mtu kama baraka da prince alitoa ngoma week 2 ilikua na view kama 2k .. huyo ndio kapotea..

Lakini kuna wasanii wao sio watu wa kutoa ngoma juu ya ngoma kama FA , AY n.k lakini sio kwamba wamepotea na siku wakitoa zinafanya vizuri tu

View attachment 1441438

Labda mimi ndo sielewi lakini kupotea ni impact tu. Mwingine anaweza kupotea baada ya kishindwa game kama ulivyosema na mwingine anaweza kupotea kama likizo tu huku anafanya issue zake nyingine..

Kupotea mimi navyoelewa ni kutokusikika kwa muda mredu hadi kuanza kusahaulika na mashabiki.

Mfano shaa amepotea lakini sio kwa sababu alishindwa muziki ila ameamua kufanya issue zingine zinazompa hela zaidi
 
Kipi huwa kinasababisha wasanii wa nyumbani wakianguka na wasiinuke tena? Tungo zao ni zilezile hawawezi kubadilisha ladha ya muziki wao au.

Ferouz alijaribu kuinuka akabaki chini pale. Q Chilla hadi leo yupo chini licha ya uwezo mkubwa wa kuimba alionao. TID naye hivyohivyo japo ukubwa wa J Nature umemsaidia hata akipata collabo anafanya kitu chenye kuonekana.

Tatizo ni nini kwa wasanii wetu ni kwamba hawana namna ya kurudi wakishuka kimuziki au mashabiki huwachoka mapema na kuwashusha wao wenyewe? Sioni Rich Mavoko akitafuna mfupa uliowashinda wengi.
Ukishafika peak basi kamwe huwez tena kuivuka ile level

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuishiwa yaani hata ukitoa ngoma haifiki popote.. mfano mavoko sasa hivi sio kwamba hatoi ngoma. Juzi kati hapo alitoa ngoma lakini haikufika popote.

Cheki mtu kama baraka da prince alitoa ngoma week 2 ilikua na view kama 2k .. huyo ndio kapotea..

Lakini kuna wasanii wao sio watu wa kutoa ngoma juu ya ngoma kama FA , AY n.k lakini sio kwamba wamepotea na siku wakitoa zinafanya vizuri tu

View attachment 1441438
Baraka nae kaisha aisee, 3weeks ana 4k views. Kweli mziki ukikutupa ni ngumu kurejea.
 
Back
Top Bottom