Harmonize kashatoka kimaisha hawezi kurudi nyuma

Mapensho star

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
3,052
Reaction score
4,104
Binafsi nampongeza kijana wangu wa Mtwara, Konde Boy kwa mafanikio aliyoyapata kupitia WCB kama kaamua kujitegemea ni jambo jema ni vema wamruhusu tu dogo akatafute sio kesi kama mkataba wake umeisha ukizingatia ni msanii aliyekuwa anaingiza mapato kuliko wasanii wote walisainiwa WCB naamini kampuni imeshanufaika vya kutosha kupitia Harmo

Huwezi kumfananisha Harmo na Rich Mavoko walivyotoka kwenye label ikumbuke Rich Mavoko alitoka kabla mkataba haujaisha bado alikuwa hajajijenga kimaisha mpaka sasa kuna uwezekano Rich Mavoko hata pesa vya kulipia video anakosa alitoka ili kuanza na yeye kusimamia wasanii akajikuta anashindwa kujisimamia yeye.

Kwa upande wa Harmo ukiangalia tayari kajijenga kimuziki na kimaisha sasa kama mtu una mili300 ndani kuna haja gani tena kuendalea kusimamiwa na kutumikishwa tumwache dogo afanye kazi zake kwa uhuru utoaji wa nyimbo WCB utagundua ni kama kutumikishwa inalazimika mara kwa mara msani awepo studio na kwenye show tofauti na wasanii wakubwa Marekani ambao wapo chini ya label mwaka mzima msanii unaweza usimsikie
 
Muda ni mwalimu sisi tupo tutaona mengi hakuna mtu anazuiliwa kutoka ila je ataweza kusimama pekee ukiangalia 90% ya mashabiki wa harmo ni wa wcb akiondoka wcb hii asilimia ya mashabiki anapoteza wcb ndio walikuwa wanampa connection na wakubwa je Leo je atakuwa na ushawishi ule ule Bila kuwa wcb? ukiangalia wcb wametengeneza mashabiki wao ndani na nje ya nchi je anaweza kupambana na fitna za mziki? Kumbuka pia harmo aliwatukana clouds media wakati akifanya show ile iliyofanyika taifa je unawezaje kupona katika mziki ukiwaumeariibu kwa wakubwa wawili wa mziki yaani wcb na clouds media kwa pamoja?
 
Wabongo ni wanafiki sana.
Yaani mnampa kichwa jamaa ili ajitoa wcb wakati mnajua kabisa akitoka anapoteza zaidi ya nusu ya mashabiki...

Kweli bongo nyoso
Huyu mtoa mada sizani hata mziki anafuatilia mziki wa Tanzania umejaa fitna nyingi ndo maana wanaofanya vizuri ni wachache japo wenye vipaji ni wengi ukiitoa wcb anaefanya vizuri Sana ni nandi na nyuma ya nandi Kuna clouds media uwezi ukasurvive Kama hauna backup yenye nguvu nyuma yako la sivyo utakuwa Kama aslay, richmavoko,Ruby,belle9,bestnaso,darassa n.k.Umeona Sasa hiv aslay analalamika mziki kuwa mgumu sijui anachukiwa pia anafanyia fitna.Huyo mmakonde ajiandae kwenda mtwara kulima asipokuwa makini.
 
Yaani wabongo bwana...
Ni kazi sana hamo kuweza kusurvive hili game la bongo...
Kwanza harmo ni mstaalabu sana kiasi kwamba hawezi kuhimili maisha ya kiki kama diamond na management ya wcb..

Na yeye kukaa ontop anasaidiwa na kiki zinazotengenezwa na management yake..

Pili inabidi watu wakubaliane tu kwamba kipaji bila figisu kwa bongo ni kazi bure tu
 
Bila shaka atakuwa kashawekeza kwenye korosho...

Farewell to HIM.
 
yawezekana umeongea ukweli kwa sehemu nyingine ila umemaliza vbaya tambua Harmonize kuondoka WCB sio kuharibu endapo atakuwa ameondoka kwa wema all in all anatakiwa ajipange
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…