Harmonize: Natamani kwenda Marekani na Rais Samia

Harmonize: Natamani kwenda Marekani na Rais Samia

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kada wa CCM na mwanamuziki wa Kizazi kipya mh Harmonize amesema baada ya Rais Samia kwenda Korea na Wasanii wa maigizo ni Imani yake safari Ijayo atasafiri na Wanamuziki wa Kizazi kipya.

Harmonize amesema yeye anatamani kwenda Marekani na Rais Samia.

==========


Msanii Staa wa Bongofleva, Harmonize amesema uamuzi wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kusafiri nao na kuwezesha Wasanii kwenda nje ya Nchi ni mzuri ambapo amesema anaamini baada ya Wasanii wa Bongomovie kwenda Korea hata Wasanii wa Bongofleva nao watapata nafasi ya kwenda Nchi mbalimbali.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo July 10,2024 Jijini Dar es salaam wakati akiitambulisha mchezo wake mpya wa Kubashiri wa Bukua Milioni, Harmonize amesema “Rais kuja kwenye uzinduzi wa Album yangu sio kwasababu yangu tu ni kwasababu Rais anatupenda Wasanii”

“Mimi natamani kwenda nje, na ofcourse lazima nitaenda nje na ukiuliza Nchi gani nitakuambia tudondoke state hapo (Marekani), Madam (Rais Samia) tupeleke zetu state, mpigie simu Mzee Biden mwambie nakuja na Vijana akina Jay Z tuwakute pale tuzungumze, si umeona akina steve wanazungumza na Wakorea”

“Mimi najua itafika wakati wa kwenda Wasanii wa Bongofleva na tutafurahi sana kama walivyofurahi Wasanii wa Bongomovie, tupo kwenye foleni yeyote atakayebahatika kwenda atakuwa ametuwakilisha wote”
 
Inawezekana zile jero zilizoongezwa kwenye luku mwezi huu ilikuwa ni kwa ajili ya kugharamia hawa maharamia
Zisiliwe tuu kwa sababu ya uchaguzi ziliwe kwa mambo yenye kuboresha hali za walalahoi,walalanjaa wa taifa hili.
 
Inamaana pamoja hela zote anazopata hawezi kwenda USA kwa hela yake.?

Au ndio yale ya ganda la ndizi?

Sasa anasemaga na anaimba sana kuwa sio unakunywa tu mapombe hujui gharama amelipa nani!!!!

Sasa na yeye asipende tu kwenda marekani hajui gharama ya nauli analipa nani!!!!

Sanaaa sayansi!!
 
Ina maana pamoja na hela zote anazopata kwenye mziki hawezi kwenda USA kwa hela yake.?

Au ndio yale ya ganda la ndizi?

Sasa anasemaga na anaimba sana kuwa sio unakunywa tu mapombe hujui gharama amelipa nani!!!!

Sasa na yeye asipende tu kwenda marekani hajui gharama ya nauli analipa nani!!!!

Sanaaa sayansi!!
 
Back
Top Bottom