Harmonize ni mnafiki sana

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Katika wasanii wa Tanzania wanaoongoza kwa unafiki basi Harmonize ni namba moja.

Jamaa ni mnafiki sana yani anajaribu kutafuta huruma ya wananchi kujifanya yeye ni mwema na kutengeneza picha mbaya kwa wenzake waonekane kama wana roho mbaya na wabinafsi.

Tangu ajitoe WCB ,watu hawana habari naye na taratibu ameshaanza kusahaulika japo hajafikisha hata mwezi jambo ambalo linamuumiza sana roho .

Miongoni mwa vitu vinavyomuumiza roho ni kitendo cha sasa hivi kufyatua fyatua nyimbo kila kukicha lakini mapokezi yamekuwa finyu sana hata zile views zimepungua kwa kasi sana.


Jamaa anatoa nyimbo ila wenzake hawamsapoti wamemuacha apambane na hali yake, sasa anajifanya ni mwema sana kwa ku repost nyimbo za wenzake ili aonekane hana kinyongo licha ya kutosapotiwa.


He he he he na bado lazima anyooke mwaka huu, hiyo ni trela tu picha halisi bado.

WCB ni kama maji usipoyanywa utayaoga.

Kitendo cha yeye kujitenga kwenye show ya wasafi na kupanda private transport ni dharau ya hali ya juu,pia kitendo cha kutoshiriki wasafi festival licha ya kushikwa mkono mpaka kufika alipofika ni ukosefu wa nidhamu sasa acha avune alichokipanda.
 
PUNGUZA CHUKI ASEE
 
Mi naona nyie ndo mwamfatilia sana
 
Unajua licha ya Clouds Fm kumshika mkono Diamond na kumfikisha mahali fulani lakini Diamond alikataa kupiga show za Clouds za Bure kisa tu eti 'walimshika mkono'.
 
Ikiwa kuna pesa/faida yoyote unayoipata kutokana na kusambaza chuki yako kwa Harmonize basi huna lawama maana hata wachawi nao wapo kutekeleza wajibu wa kazi zao. Na ikiwa huna chochote ukipatacho cha faida nyuma ya chuki yako hii basi wewe ni moja kati ya mashabiki maandazi wasioutakia mema mziki wetu.
UNAJUA ULICHOKIANDIKA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…