Nawasalimu wana Jamiiforums
Nimeona ni Busara kutoa ufafanuzi hapa jukwaani na kuweka kumbukumbu sawa katika jambo hili la ujenzi wa stand ya Mbezi Luis, Mradi huo ulikuwa na thamani ya sh 51 billion na mkata huo ulisainiwa mwaka Jana 2019 February, Mradi huu ungepaswa kukamilika July 15, 2020
Sisi jiji tulichangia sh 11.5 (thamani ya Kiwanja) ambayo ni pesa zilizo lipwa kwa wananchi wa hapa mbezi
Malipo hayo yamefanyika kwa phase II
Phase II Malipo yalio lipwa na watangulizi wangu ambao waliwalipa wananchi hao mwaka 1998 - 2000 Zaidi ya sh 3 billion
Phase II Malipo tuliyo yalipai sh 8.7 billion kwa mwaka wa 2018
Mwaka 2018 serikali kwa kupitia wizara yake ya Tami semi walikuja na wazo la Miradi ya kimkakati na kwamba serikali ilikuwa inazipa Halmashauri pesa kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii na sisi jiji tulinufaika na mpango huu na serikali ilitupa sh 51billion ili kuweza kujenga mradi huu , isipo kuwa fedha hizo zilibaki chini ya uwangalizi wa wizara ya fedha na sisi jiji wajibu wetu mkubwa ulikuwa ni usimamizi tuu ila mlipajii mkuu alibaki kuwa wizara ya fedha
Kama nilivyo sema hapo juu mradi huu ungekamilika July 2020 .... sasa kabla ya muda huo kutimia tayari mimi nilikwisha ondolewa ofisini na sikujua nini kilisababisha mrad huoi kutokamilika kwa Muda .. Nafikiri kwamba watumishi wetu wa jiji pamoja na wizara ya fedha wanaweza kuwa na majibu mazuri katika jambo hili
Pia ndugu zangu ni vizuri mkajua ni kwanini miradi mingi ya serikali hupata variation ... sababu kubwa ziko wazi kabisa...