Haruna Moshi Bobani

Haruna Moshi Bobani

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
HARUNA MOSHI MNYAMWEZI WA TABORA 'SHILLING 10' KWENYE KIOO CHA ZVONMIR BOBAN
.
1987 katikati mwa Tanzania, pale Mboka Manyema kwa Wastaarabu wa Kinyamwezi, pale maskani ya Chief Mirambo, ndipo hapo alipotoka fundi mmoja wa mpira aliyefunga ndoa na soka, alieweka nadhiri ya kuwapa burudani ya soka Watanzania, lipa elfu 3 mengine mwachie yeye
.
Wakati 2004 anaingia makutano ya Uhuru na Msimbazi, wenyewe mnapaita Kariakoo, wenyewe mnapaita nyumbani kwa Simba, pale palipo Makao makuu ya Barcelona ya Bongo, Simba ile iliyokuwa na majina Kama Ulimboka Mwakingwe 'VCD', Joseph Kaniki 'Golota' tulia kidogo, ni Simba ile ya computed footballers watu walikuwa wakienda uwanjani mnaambiwa msisahau net maana soka la Mnyama ni kama lullaby songs, utalala
.
Haruna ndani ya Simba alipewa ile '10 role' pale mitaa ya wahuni wangu Tabata Dampo wanaita shilling 10, kazi yake ni kupika, kuunganisha na kufunga, wasomi wa Biologia vuteni picha tu kazi ya Mitochondria kwenye Cell, basi Haruna alikuwa Mitochondria ya burudani za Simba, jukwaa gani kwa Mkapa lilikuwa halinyanyuki akiwa na mpira?, Killer passes, nywele zake hazijali sana, hawajali sana watu jukwaani yeye anamjali namba 9 wake pale mbele
.
Unataka useme Nini mpaka akapewa jina la mchawi mmoja ZVONMIR BOBAN, mwamba kutoka Croatia, mchawi wa kusambaza burudani pale San Siro, waitaliano walikuwa wanamuita the Croatian Maestro, wabongo tukampa Haruna, zile exquisite techniques, field vision, ball control na set pieces specialist, Haruna MOSHI wa TABORA
.
Kuna uhusiano gani Kati ya jina la Haruna na soka?? Kuna uhusiano gani Kati ya Haruna wa Gisenyi na Haruna wa TABORA? Ni maswali Hatuna majibu, tupeni four figure tusake hiyo 'X' Haruna aliwafanya Waswidi pale kwa Zlatan walie, Gefle IF wanakumbuka burudani za muhuni mstaarabu, wazungu waliona jamaa ataenda ligi kubwa Ulaya Ila haikuwa hivyo, Nini kilitokea anajua Haruna na Mungu wake.
IMG-20191228-WA0004.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiniambia boban ana miaka 32 nakataa katakata na ukinilazimisha omba Mungu niwe sijalewa pombe nitakukata kibao kimoja kikali sana
 
Huyu Alibweteka sana na ustaa wa kibongo
Alipopata nafasi ya kwenda kucheza nje
Alitakiwa akomae....akalilia arudi bongo anadai Maisha ulaya ni ya upweke
Mwisho wa siku tukawa tunashinda naye mawela sinzaaaa
Boban ni kipaji kilichopoteaaa

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Chini kidogo kuna pusha mshona viatu watu wanamaliza
 
Umeyataja hayo mjina kwa vile unawafahamu hao watu. Hebu nipe hiyo link ya boban na kiombe Dr.
Walikua wanakutana wapi kwa issue gani? Lbd zembwel mtu wa wtu.
Iko hivi Boban hatakagi kuongea sana ila issue yake yakurudi bongo aliamua kumkomesha ndumbaro aliyekua anakula kupitia jasho la haruna huku haruna akishindwa hata kumudu mahitaji yake.
Bongo hatuna waandishi wazuri ndo maana haya hatuyajui kiundani.
kwa kina god na mlevi kiombe na rafiki yake chuji na bange sinza star pamoja na zembwela ,teh teh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeyataja hayo mjina kwa vile unawafahamu hao watu. Hebu nipe hiyo link ya boban na kiombe Dr.
Walikua wanakutana wapi kwa issue gani? Lbd zembwel mtu wa wtu.
Iko hivi Boban hatakagi kuongea sana ila issue yake yakurudi bongo aliamua kumkomesha ndumbaro aliyekua anakula kupitia jasho la haruna huku haruna akishindwa hata kumudu mahitaji yake.
Bongo hatuna waandishi wazuri ndo maana haya hatuyajui kiundani.

Sent using Jamii Forums mobile app
god alikuwa mmoja wa wamiliki wa mawela ,kiombe ni mlevi maarufu hapo,,so ukienda hapo. automatically utakuwa unadance nao
 
HARUNA MOSHI MNYAMWEZI WA TABORA 'SHILLING 10' KWENYE KIOO CHA ZVONMIR BOBAN
.
1987 katikati mwa Tanzania, pale Mboka Manyema kwa Wastaarabu wa Kinyamwezi, pale maskani ya Chief Mirambo, ndipo hapo alipotoka fundi mmoja wa mpira aliyefunga ndoa na soka, alieweka nadhiri ya kuwapa burudani ya soka Watanzania, lipa elfu 3 mengine mwachie yeye
.
Wakati 2004 anaingia makutano ya Uhuru na Msimbazi, wenyewe mnapaita Kariakoo, wenyewe mnapaita nyumbani kwa Simba, pale palipo Makao makuu ya Barcelona ya Bongo, Simba ile iliyokuwa na majina Kama Ulimboka Mwakingwe 'VCD', Joseph Kaniki 'Golota' tulia kidogo, ni Simba ile ya computed footballers watu walikuwa wakienda uwanjani mnaambiwa msisahau net maana soka la Mnyama ni kama lullaby songs, utalala
.
Haruna ndani ya Simba alipewa ile '10 role' pale mitaa ya wahuni wangu Tabata Dampo wanaita shilling 10, kazi yake ni kupika, kuunganisha na kufunga, wasomi wa Biologia vuteni picha tu kazi ya Mitochondria kwenye Cell, basi Haruna alikuwa Mitochondria ya burudani za Simba, jukwaa gani kwa Mkapa lilikuwa halinyanyuki akiwa na mpira?, Killer passes, nywele zake hazijali sana, hawajali sana watu jukwaani yeye anamjali namba 9 wake pale mbele
.
Unataka useme Nini mpaka akapewa jina la mchawi mmoja ZVONMIR BOBAN, mwamba kutoka Croatia, mchawi wa kusambaza burudani pale San Siro, waitaliano walikuwa wanamuita the Croatian Maestro, wabongo tukampa Haruna, zile exquisite techniques, field vision, ball control na set pieces specialist, Haruna MOSHI wa TABORA
.
Kuna uhusiano gani Kati ya jina la Haruna na soka?? Kuna uhusiano gani Kati ya Haruna wa Gisenyi na Haruna wa TABORA? Ni maswali Hatuna majibu, tupeni four figure tusake hiyo 'X' Haruna aliwafanya Waswidi pale kwa Zlatan walie, Gefle IF wanakumbuka burudani za muhuni mstaarabu, wazungu waliona jamaa ataenda ligi kubwa Ulaya Ila haikuwa hivyo, Nini kilitokea anajua Haruna na Mungu wake.View attachment 1305912

Sent using Jamii Forums mobile app
1987 hapo umetudanganya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani huko ulaya kuna bangi? Lazima awe mpweke sasa wewe upo upo tu kule hawana muda, wenzie wanawaza maisha yeye anawaza ndumu wapi na wapi lazima arudi[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom