Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
HARUNA MOSHI MNYAMWEZI WA TABORA 'SHILLING 10' KWENYE KIOO CHA ZVONMIR BOBAN
.
1987 katikati mwa Tanzania, pale Mboka Manyema kwa Wastaarabu wa Kinyamwezi, pale maskani ya Chief Mirambo, ndipo hapo alipotoka fundi mmoja wa mpira aliyefunga ndoa na soka, alieweka nadhiri ya kuwapa burudani ya soka Watanzania, lipa elfu 3 mengine mwachie yeye
.
Wakati 2004 anaingia makutano ya Uhuru na Msimbazi, wenyewe mnapaita Kariakoo, wenyewe mnapaita nyumbani kwa Simba, pale palipo Makao makuu ya Barcelona ya Bongo, Simba ile iliyokuwa na majina Kama Ulimboka Mwakingwe 'VCD', Joseph Kaniki 'Golota' tulia kidogo, ni Simba ile ya computed footballers watu walikuwa wakienda uwanjani mnaambiwa msisahau net maana soka la Mnyama ni kama lullaby songs, utalala
.
Haruna ndani ya Simba alipewa ile '10 role' pale mitaa ya wahuni wangu Tabata Dampo wanaita shilling 10, kazi yake ni kupika, kuunganisha na kufunga, wasomi wa Biologia vuteni picha tu kazi ya Mitochondria kwenye Cell, basi Haruna alikuwa Mitochondria ya burudani za Simba, jukwaa gani kwa Mkapa lilikuwa halinyanyuki akiwa na mpira?, Killer passes, nywele zake hazijali sana, hawajali sana watu jukwaani yeye anamjali namba 9 wake pale mbele
.
Unataka useme Nini mpaka akapewa jina la mchawi mmoja ZVONMIR BOBAN, mwamba kutoka Croatia, mchawi wa kusambaza burudani pale San Siro, waitaliano walikuwa wanamuita the Croatian Maestro, wabongo tukampa Haruna, zile exquisite techniques, field vision, ball control na set pieces specialist, Haruna MOSHI wa TABORA
.
Kuna uhusiano gani Kati ya jina la Haruna na soka?? Kuna uhusiano gani Kati ya Haruna wa Gisenyi na Haruna wa TABORA? Ni maswali Hatuna majibu, tupeni four figure tusake hiyo 'X' Haruna aliwafanya Waswidi pale kwa Zlatan walie, Gefle IF wanakumbuka burudani za muhuni mstaarabu, wazungu waliona jamaa ataenda ligi kubwa Ulaya Ila haikuwa hivyo, Nini kilitokea anajua Haruna na Mungu wake.
Sent using Jamii Forums mobile app