Harusi ya binti wa Dangote yafana! Yahudhuriwa na vigogo wakiwemo Bill Gates na Jakaya Kikwete

kadoda11

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
21,453
Reaction score
20,746
Inasemekana matajiri wengi wakubwa wa level ya Forbes akiwemo Bill Gates na watu mbalimbali mashuhuri duniani walihudhuria.

Kwa mujibu wa mtangazaji wa runinga nchini Kenya, ndugu Jeff Koinange, anasema hata mzee wetu kipenzi Rais mstaafu wa Tanzania mzee Jakaya Kikwete alihudhuria.

Picha kwa msaada wa mtandao wa Instagram.

--------
TAARIFA ZAIDI..

Sherehe ya kifahari ya binti wa Bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote aitwaye Fatima Dangote, yazua gumzo nchini humo kutokana na kuhudhuriwa na watu mashuhuri kutoka sehemu mbalimbali duniani akiwemo Bilionea kutoka Marekani, Bill Gates.

Naye Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete alikuwa ni miongoni mwa wageni wa heshima waliohudhuria katika sherehe hiyo ya kihistoria.

Wengine walioudhuria ni pamoja na mke wa Rais wa sasa wa Nigeria, Hajiya Aisha Buhari; Makamu wa Rais, Osinbanjo; Spika wa Bunge, Magavana na Watu wengine mashuhuri wakiwemo wasanii na wafanyabiashara wakubwa.

Davido na Wizkid waliangusha show moja kali sana mpaka mzee Dangote mwenyewe ikambidi ayarudi magoma.

Tafrija hiyo ya mapokezi baada ya ndoa (reception party) kati ya Fatima na mumewe ambaye ni mtoto wa Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, Jamilu Abubakar, ilifanyika jana Ijumaa katika Jiji la Lagos.



 

Attachments

  • IMG_20180324_150229.jpg
    61.6 KB · Views: 521
  • 68676d697c73abc5ba3d8b8e2241ec55.jpg
    47.1 KB · Views: 502
  • 6280e37e4c1dd28f54b6baf6201db563.jpg
    74.6 KB · Views: 493
  • 38f75d836816f3c7a4eb1238a9878abb.jpg
    39.5 KB · Views: 495
  • 0b7764e2d1c53e3634ca6e015af1eded.jpg
    47.2 KB · Views: 503
  • 4d5a77c8ecfcc2fcb6e05e9edc1c191e.jpg
    10.4 KB · Views: 505
  • 0c235fe3368022a1265b3c1a69e0b733.jpg
    73.7 KB · Views: 463
  • 2b1aa699a554ceef311a2a318c34153d.jpg
    120.3 KB · Views: 510
  • 11c76c3e1a59ef32bee89cb953a84ea5.jpg
    126 KB · Views: 480
  • 752e1e9a738236010972400147560fe3.jpg
    85.2 KB · Views: 484
  • 77d49763a5c8bd1d6a6b7ee113b78eaf.jpg
    78.6 KB · Views: 507
  • d752b38b5535aef218555f6b0f260df4.jpg
    85.2 KB · Views: 503
haka kabibi harus kamebeba ugonjwa wangu..(MWANYA)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…