Inasikitisha kuona watu, wengine wanaume wazima (afadhali hata sisters unaweza kusema wanatetea maslahi yao katika kutaka kuolewa) wanamsema vibaya mtu mume mwenzao kwenye ndoa yake kwa specualations na umbea. Kila mtu na maisha yake, haya mambo mengine ni ufinyu wa mawazo tu. Kama wameoana kwa hili, au lile ni mambo yao wawili, uchimvi mwingi unakuwa umbeya tu. Mauritania huko mwanamke asipokuwa mnene hapati mume, wanawake wanashindana unene. Sasa kama mazee ndiyo mapigo yake mnataka kumlazimisha types asizozitaka ?
Mnataka kupangia watu kuoa sasa? Ndiyo maana wengine hatuoi, usipooa mineno, ukioa mineno, basi tabu tupu.
Wanaume wazima mnamsema mwenzenu kaoa mlitaka awaoe nyie? Huyo boflo tunamjua, na nyie wengine je ?
Mimi sijui hii ndoa imepitia mambo gani, wamesaidiana vipi, wamependana vipi mpaka kufikia sakrameti hii takatifu, kwa hiyo naona jambo la kheri tu.Mwacheni mtu katika maisha yake, mimi ninamtakia kheri katika ndoa yake tu. Uungwana hauuzwi dukani.
Type zingine hapa zinaweza hata kupekua garbage kuangalia kama mmekula kizuri au kibaya. Hatari.