Dar es salaam kila kitu ni ujanja ujanja, anzia magengeni tunalishwa taka taka nyingi mno, maharusini ndio kabisaa alafu kule huwa wanaweka oda kuilisha harusi nzima,
Hapo ndipo uchakachuzi hufanyika.. juzi nilikuwa kwenye sherehe kiukweli kuku na nyama tuliolishwa nilistukia yaani haina radha kabisa,
USHUHUDA
Nilitoka kwetu mikoani enzi zile nikiwa na afya njema, sasa kutokana na majukumu mengi nikawa nakula magengeni, nilikula kwa mwaka mzima,
Kilicho nikuta sitakisahau niliugua macho, miguu, masikio halafuu nilikonda balaaa,
Nilienda pale CCBRT kutibiwa macho nikapigwa dozi ya miezi mitatu wala siakupona, nikaenda sinza, mwananyamala kote sikufanikiwa kupona,
Mwishoni nilikutana na daktari mmoja kutoka pale muhimbili , huyu ndiye aliye niponyesha tatizo ilikuwa ni upungufu wa VIRUTUBISHO MWILINI alinipa dawa na ushauri .
Nilipona na namshukuru sana yule mama mungu ambariki .
USHAURI
Usipende sana kula magengeni na maharusini mara kwa mara hapa dsm.